ARSENAL, MAN CITY, LIVERPOOL ZAMGOMBEA KINDA WILFRIED ZAHA

Arsenal, Liverpool na Manchester City zitatakiwa kulipa angalau Pauni Milioni 20 kama zinataka kumsajili kinda wa Crystal Palace mwenye umri wa miaka 19, winga Wilfried Zaha.
Birmingham itatakiwa kuwauza Jack Butland, mwenye umri wa miaka 19, na Nathan Redmond, mwenye miaka 18, vinginevyo wapate mmiliki mpya. Everton na Southampton zimekuwa zikihusishwa na mpango wa kumsajili kipa Butland, wakati winga Redmond anaweza kuwa anatakiwa na Manchester City.

WACHEZAJI ENGLAND WAPEWA VIDONGE VYA USINGIZI

Baadhi ya wachezaji wa England, walihitaji vidonge vya usingizi baada ya mechi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Poland kuchelewa kwa saa 20 kutokana na mvua kubwa.
Chama cha Soka kimetoa ripoti kuhusu timu ya vijana ya England chini ya miaka 21 dhidi ya Serbia kikisema matatizo yalianza hata kabla ya mechi kuanza.
Mshambuliaji wa zamani wa Aston Villa na Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya Serbia chini ya miaka 21, Savo Milosevic, nchi hiyo inahitaji msaada kutatua matatizo yake.
Kiungo wa Manchester City, David Silva, mwenye umri wa miaka 26, anaweza kuwa nje ya Uwanja kwa wiki tatu baada ya kuumia nyama za paja akiichezea Hispania katika mechi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa .

NILE RANGE WIKI SITA NJE

Kocha wa Newcastle, Alan Pardew amesema mshambuliaji Nile Ranger, mwenye umri wa miaka 21,hawezi kurejea kikosi cha kwanza hadi baada ya wiki sita.