ARSENAL KUSAJILI BONGE LA STRIKER LA BUNDESLIGA

KIPA WA BIRMINGHAM KUUZWA ATAKE ASITAKE

KIPA wa Birmingham City, Jack Butland amesema kwamba atauzwa atake asitake, ikiwa wamiliki wa klabu hiyo hawatatua matatizo yao Januari. Kipa huyo chipukizi mwenye umri wa miaka 19 ameripotiwa kuivutia klabu ya Ligi Kuu England, Everton.
Jack Butland and Danny Rose
Jack Butland (kulia) ameichezea England kuanzia U16 hadi timu ya wakubwa
Liverpool hatimaye imejipanga kumsaini mshambuliaji wa HJK Helsinki, Joel Pohjanpalo  baada ya kuboresha ofa yake kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18, ambaye amefunga mabao 19 katika mechi 34 za kikosi cha kwanza cha HJK.
Chelsea na Manchester City zote zinamtolea macho kipa wa Obolon Kiev, Igor Berezovsky baada ya mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 22 kuonyesha uwezo mkubwa katika Daraja la Kwanza Ukrainie.
Arsenal inataka kumsajili mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Andre Schurrle ifikapo Januari. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ni mmoja kati ya wachezaji watatu wa Bundesliga wanaotakiwa, wengine wakiwa ni kiungo wa Schalke, Lewis Holtby, mwenye miaka 22, na mshambuliaji wa Hamburg, Heung-Min Son, mwenye miaka 20, ambao pia wanaweza kuondoka.