// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ANA KWA ANA NA MILOVAN, ASEMA SASA HAKUNA KULALA NA MAPIGANO KWA KWENDA MBELE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ANA KWA ANA NA MILOVAN, ASEMA SASA HAKUNA KULALA NA MAPIGANO KWA KWENDA MBELE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, October 18, 2012

    ANA KWA ANA NA MILOVAN, ASEMA SASA HAKUNA KULALA NA MAPIGANO KWA KWENDA MBELE

    Profesa Milovan Cirkovick

    BAADA ya Simba kutoa sare ya pili mfululizo jana katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, BIN ZUBEIRY leo amefanya mahojiano na kocha wa Wekundu hao wa Msimbazi, Profesa Milovan Cirkovick, raia wa Serbia kuhusu masuala mbalimbali juu ya timu yake. Endelea.
      
    BIN ZUBEIRY: Habari za leo kocha
    PROF MILOVAN: Nzuri, sema

    BIN ZUBEIRY: Nina maswali machache nataka kukuuliza kuhusu timu
    PROF MILOVAN: Uliza

    BIN ZUBEIRY: Hatumuoni Abdallah Juma hata benchi, ana tatizo gani?
    PROF MILOVAN: Abdallah alikuwa nje ya timu (alisafiri) kwa zaidi ya wiki moja hakufanya mazoezi na timu, ila amerudi na ameanza mazoezi, akiwa vizuri atapangwa

    BIN ZUBEIRY: Na katika mechi mbili zilizopita, Edward Christopher hakucheza, wakati amekuwa akicheza vizuri siku za karibuni
    PROF MILOVAN: Kweli, nilimpumzisha ili nitumie na wachezaji wengine pia na kama jana kulikuwa kuna Okwi na Ngassa, unadhani ningemuacha nani kati yao nikampanga yeye

    BIN ZUBEIRY: Hata kuingia akitokea benchi ilishindikana?
    PROF MILOVAN: Ungekuwa wewe ungemtoa nani ukamuingiza Edward kati ya Okwi na Ngassa

    BIN ZUBEIRY: Nadhani Okwi jana hakuwa vizuri sana
    PROF MILOVAN: Okwi ni mtu ambaye wakati wowote huwa natarajia kitu kutoka kwake, wakati wowote anaweza akabadilisha matokeo ya mchezo

    BIN ZUBEIRY: Na siku za karibuni, Amri Kiemba humtumii kama kiungo mkabaji tofauti na mwanzoni mwa msimu
    PROF MILOVAN: Unataka kuingilia kazi yangu sasa, wewe ni kocha?

    BIN ZUBEIRY: Na jana pia hatukumuona kijana Shomary Kapombe pale nyuma, si kawaida, vipi?
    PROF MILOVAN: Kapombe anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu ndiyo maana hukumuona hata benchi jana

    BIN ZUBEIRY: Na unayazungumziaje matokeo ya jana kwa ujumla, ukiwa umetoa sare ya pili mfululizo
    PROF MILOVAN: Ndiyo mpira, mimi na wachezaji wangu tumejifunza kitu na hatutarajii kurudia makosa

    BIN ZUBEIRY: Umewasogeza karibu sana Azam, na Yanga sasa hawako mbali na wewe
    PROF MILOVAN: Azam kweli wapo karibu na sisi, lakini tutaongeza juhudi sasa, wachezaji wangu na mimi sasa hivi tunaona umuhimu wa kujitolea zaidi

    BIN ZUBEIRY: Mechi ijayo unarudi Tanga Jumapili kwenye Uwanja mbaya, unasemaje
    PROF MILOVAN: Kweli, ni hali halisi, tutakwenda kupigana kwa vyovyote tushinde, hatutaki matokeo kama haya tena

    BIN ZUBEIRY: Mwanzoni, kila baada ya mechi ulikuwa unasema kama kawaida, maana yake ushindi, lakini sasa unaizungumziaje ligi
    PROF MILOVAN: Ni nzuri, ngumu na ina changamoto ya kutosha

    BIN ZUBEIRY: Timu ipi unaihofia zaidi
    PROF MILOVAN: Kila timu inawania ubingwa, kila timu ni mpinzani

    BIN ZUBEIRY: Kuna ambayo ni mpinzani zaidi, ipi?
    PROF MILOVAN: Wazi ni Azam na Yanga

    BIN ZUBEIRY: Asante kocha, nakutakia siku njema na kazi njema
    PROF MILOVAN: Asante, na wewe pia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ANA KWA ANA NA MILOVAN, ASEMA SASA HAKUNA KULALA NA MAPIGANO KWA KWENDA MBELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top