MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Togo, Emmanuel Adebayor anajiandaa kuondoka Tottenham ifikapo Januari, mwakani sasa ikiwa ni mwezi mmoja tu tangu asaini mkataba wa kudumu na klabu hiyo.
Adebayor anataka kuondoka Spurs baada ya kushindwa kumridhisha kocha Andre Villas-Boas, ambaye anamuweka benchi.
Mshambuliaji huyo alipigwa 'mkeka' wakati Spurs ikilala 4-2 mbele ya Chelsea jana na hiyo imedhihirisha sasa ameamua kukubali yaishe.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, amefunga mabao 17 katika mechi 32 za Ligi Kuu msimu uliopita, lakini msimu huu ameingia mara tatu tu akitokea benchi chini ya AVB.
Emmanuel Adebayor yupo katika wakati mgumu msimu huu