Kikosi cha Yanga kilichomenyana na JKT, kutoka kulia waliosimama Berko, Yondan, Chuji, Kavumbangu, Joshua, na Cannavaro. Waliopiga magoti kutoka kulia ni Twite, Kiiza, Msuva, Niyonzima na Nizar. |
Na Mahmoud Zubeiry
YANGA iko
hatarini kupokonywa pointi tatu ilizovuna kutokana na ushindi wa mabao 4-1
dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutokana na
kuzidisha idadi ya wachezaji wa kigeni.
Mwenyekiti wa
Kamati ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Wallace Karia ameiambia BIN
ZUBEIRY mida hii kwamba, klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji watano wa
kigeni, lakini itaruhusiwa kutumia watatu tu kwa wakati mmoja.
Alisema mabadiliko
ya kanuni za wachezaji wa kigeni, kutoka watano hadi 10 kusajiliwa na watano
kucheza kwa wakati mmoja, yataanza kutumika msimu ujao.
“Tunatarajia
kukutana keshokutwa kupitia ripoti za mechi zote, ikiwemo mechi ambayo Emmanuel
Okwi alimpiga mchezaji mwenzake ngumi, baada ya kikao tutatoa ripoti ya
maamuzi,”alisema Karia.
Jumamosi,
Yanga ikimenyana na JKT Ruvu, Mgahan Yawe Berko, alianza langoni, Wanyarwanda
Mbuyu Twite alicheza beki ya kulia, Haruna Niyonzima alicheza kiungo cha juu,
Mrundi Didier Kavumbangu na Mganda Hamisi Kiiza walicheza mbele.
Kikosi
cha Yanga siku hiyo kilikuwa; Yaw Berko, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir
Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Nizar Khalfan/Shamte
Ally, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbangu/Jerry Tegete, Hamisi Kiiza na Simon
Msuva.Uzembe huu, moja kwa moja unatokana na mabadiliko yaliyofanywa Ijumaa, kumuondoka Meneja wa timu, Hafidh Saleh bila kuteua Meneja mpya na pia unadhihirisha ukosefu wa umakini wa benchi la ufundi la sasa, chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Freddy Felix Minziro, anayekaimu nafasi hiyo baada ya kufukuzwa kwa Mbelgiji, Tom Saintfiet.
0 comments:
Post a Comment