|
Yanga wakishangilia bao la ushindi la Bahanuzi |
|
Bahanuzi kulia akitafuta mbinu za kumtoka Nahodha wa Coastal, Saidi Swedi |
|
Said Bahanuzi 'Spider Man' |
|
Kikosin cha Coastal |
|
Kaira akiwa amelala baada ya kujifunga, kulia ni kipa Juma Mpngo akimuangalia kwa 'hasira' |
|
Kocha Saintfiet akiwapa mawaidha wachezaji wake, wakati huo bado wako nyuma kwa 1-0 |
|
Mohamed Binslum, mmoja wa wachezaji wa Coastal |
|
Kocha Mgunda akizungumza na marefa wakati wa sakata la mgomo |
|
Msuva aliyekaa chini- hapa alikosa bao la wazi |
|
Mwasyika kulia akifumua shuti |
|
Mwasyika akipita kulia, kushoto ni Saidi Swedi |
|
Kaira kushoto akimdhibiti Bahanuzi |
|
Razack Khalfan, mfungaji wa bao la Coastal |
|
Seif Ahmad 'Magari', kigogo wa usajili Yanga, akizungumza na mwandaaji wa mechi ya leo, Bonga, kushoto ni Katibu wa Yanga, Celestine Mwesigwa |
|
Kocha Saintfiet katikati na Msaidizi wake, Freddy Felix Minziro kulia wakimsihi kocha wa Coastal, Juma Mgunda aingize timu mapema mechi ianze |
|
Sainftiet anatoa timu uwanjani |
|
WOTE NJE; Sainftiet akiwaamrisha wachezaji wake kutoka |
|
Kikosi cha Yanga kilichoanza |
|
Yangab wakiwa chumbani kwao kabla ya kurejea kucheza |
Na
Mahmoud Zubeiry
MABAO
mawili ya dakika za lala salama, leo yameinusuru Yanga SC kulala mbele ya Coastal
Union ya Tanga, baada ya kushinda 2-1 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Saidi
Bahanuzi ‘Spider Man’, kwa mara nyingine leo alikuwa shujaa wa Yanga baada ya
kufunga bao la ushindi dakika ya 85 katika mchezo, ambao Coastal Union ilimpoteza
kiungo wake Jerry Santo aliyepewa kadi nyekundu kwa kumtolea maneno machafu
refa Hashim Abdallah dakika ya 59.
Hilo
lilikua bao lake la nane Bahanuzi tangu aanze kuichezea Yanga miezi miwili
iliyopita, akitokea Mtibwa Sugar. Awali ya hapo, beki Mganda, Philip Kaira
alijifunga katika harakati za kuokoa krosi ya Shamte Ally dakika ya 84.
Hadi
mapumziko, Coastal tayari walikuwa mbele kwa bao hilo moja lililotiwa kimiani
na kiungo Razack Khalfan, aliyefumua shuti la umbali wa mita 26.
Razack
alitokea Yanga B mwaka 2008 na kupandishwa kikosi cha kwanza mwaka 2009, chini
ya kocha Mserbia, Profesa Dusan Savo Kondic, lakini misimu miwili baadaye
akatolewa kwa mkopo African Lyon, ambao umeisha na msimu huu amesaini Coastal.
Kwa
ujumla Razack, mdogo wa kiungo wa Yanga, Nizar Khalfan alicheza soka ya
kusababisha swali kwa nini Yanga ilimuacha.
Mechi
hiyo ilichezeshwa na refa Hashim Abdallah aliyechezesha pia mechi ambayo Yanga
ililala 5-0 kwa Simba katika Ligi Kuu msimu uliopita, ambaye leo amesaidiwa na
Shaffi Mohamed na Iddi Maganga.
Awali,
mchezo huo nusura uvunjike, baada ya kocha wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet
kutoa timu uwanjani kutokana na kucheleweshwa kwa muda wa kuanza, ambao
kimakubaliano ulikuwa saa 10:00 jioni.
Lakini
Coastal walichelewa kufika uwanjani (walifika saa 10:05 jioni ) na kuanza
kwanza kupasha misuli moto, jambo ambalo lilimkera Saintfiet na kusistiza
waachane na mazoezi yao mechi ianze, lakini makocha wa timu hiyo ya Tanga, Juma
Mgunda na Habib Kondo waliendelea na biashara yao.
Saintfiet
akatoa timu yake uwanjani, kabla ya kwenda kubembelezwa na viongozi wake, ndipo
akarejesha timu na mpira ukaanza saa 10:31 jioni.
Kwa
ujumla Coastal walitawala kipindi cha kwanza mchezo huo na kipindi cha pili
japokuwa mchezo ulikuwa wa pande zote mbili hata baada ya Santo kutolewa kwa
kadi nyekundu, lakini Yanga waliuteka kabisa dakika 15 za mwishoni.
Kwa
Coastal, hiyo inakuwa mechi ya nne Coastal wanafungwa ndani ya mechi tano za
kujipima nguvu, nyingine zikiwa dhidi ya Bandari mara mbili, 3-2 Mombasa na 2-0
Tanga na 2-1 dhidi ya Polisi mjini Morogoro, wakati mechi waliyoshinda ni dhidi
ya JKT Oljoro 2-0.
Kwa
Yanga, chini ya kocha wake Mbelgiji, Saintfiet, hiyo inakuwa mechi ya 10 anashinda
kati ya 11 alizocheza tangu ajiunge na kabu hiyo miezi miwili iliyopita.
Yanga
SC;
Ally Mustafa ‘Barthez’ (1), Juma Abdul (14)/Frank Domayo(18), Oscar Joshua (4)/Shamte
Ally (15), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (23), Kelvin Yondan (5), Mbuyu Twite (9),
Simon Msuva (27), Haruna Niyonzima (8), Said Bahanuzi (11)/Geoffrey Taita (17),
Didier Kavumbangu (21)/Jerry Tegete (10) na Stefano Mwasyika (3)/David Luhende
(29).
Coastal
Union; Juma
Mpongo (1), Saidi Swedi (26), Juma Jabu (15), Cyrprian Lukindo (27), Philip
Kaira (18), Jerry Santo (6), Soud Mohamed (8)/, Salum Aziz Gilla (19), Razack
Khalfan (28), Nsa Job (29), Atupele Green (3)/Dajnny Lyanga (16)na Suleiman
Kassim ‘Selembe’ (25).
0 comments:
Post a Comment