Kavumbangu alifunga mabao mawili Yanga na JKT Ruvu |
Na Mahmoud Zubeiry
MECHI za
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara za Simba na Yanga zilizochezwa wikiendi
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zimeshuhudiwa na washabiki 65,458.
Ofisa Habari
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo, ameiambia BIN
ZUBEIRY mida hii kwamba, Yanga ambayo iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya
JKT Ruvu, Jumamosi , mechi yao ilishuhudiwa na washabiki 15,770 wakati ile ya
Simba na Ruvu Shooting iliyochezwa jana (Septemba 23 mwaka huu) ilikuwa na
washabiki 9,688. Simba ilishinda mabao 2-1.
Amesema mechi
ya Yanga iliingiza sh. 88,251,000 ile ya Simba dhidi ya Ruvu Shooting Stars
mapato yalikuwa sh. 55,454,000. Mechi ya Yanga kila timu ilipata sh.
19,846,194.92 huku ile ya Simba kila timu ilipata sh.11,350,774.58.
Kuhusu mechi
ya Azam na Mtibwa Sugar iliyochezwa juzi Uwanja wa Chamazi, Wambura amesema imeingiza
sh. 2,509,000 ambapo kila timu imepata mgawo wa sh. 301,661.
Amesema Washabiki
827 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyomalizika kwa Azam kuibuka na
ushindi wa bao 1-0, wakati mechi ya ligi hiyo kati ya African Lyon na Tanzania
Prisons iliyochezwa jana, kwenye uwanja huo imeingiza sh. 245,000 huku kila
timu ikipata sh. 32,286. Prisons ilishinda mechi hiyo kwa mabao 2-1.
Wakati huo
huo: TFF imetoa pongezi kwa uongozi mpya wa vyama vya mpira wa miguu mikoa ya
Kilimanjaro (KRFA) na Manyara (MARFA) katika uchaguzi uliofanyika juzi.
TFF imesema
ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza vyama hivyo unaonesha jinsi
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa KRFA na ule wa MARFA walivyo na imani kubwa kwao
katika kusimamia mchezo huo katika mikoa hiyo.
TFF inaahidi
kuendeleza ushirikiano wake kwa kamati za utendaji za MARFA na KRFA
zinazoongozwa na Elley Mbise na Goodluck Moshi, kwani viongozi hao wapya wana
changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha wanaendesha shughuli za mpira wa
miguu kwa kuzingatia katiba zao na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yao.
TFF pia imetoa
pongezi kwa Kamati za uchaguzi za IRFA na MARFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF
kwa kuhakikisha uchaguzi unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za
wanachama wa TFF.
Viongozi
waliochaguliwa kuongoza MARFA ni Elley Mbise (Mwenyekiti), Wilson Ihucha
(Makamu Mwenyekiti), Apollinary Kayungi (Katibu), Peter Abong’o (Mhazini),
Khalid Mwinyi (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Phortinatus Kalewa (Mwakilishi wa
Klabu TFF) na Peter Yaghambe (Mjumbe).
Kwa upande
wa KRFA waliochanguliwa ni Goodluck Moshi (Mwenyekiti), Mohamed Musa (Katibu),
Kenneth Mwenda (Mwakilishi wa Klabu TFF), Kusiaga Kiyata (Mhazini) na Denis
Msemo (Mjumbe). Nafasi zilizowazi baada ya kukosa wagombea wenye sifa kwenye
vyama hivyo zitajazwa baadaye.
0 comments:
Post a Comment