|
Wachezaji wa Yanga, wakimpongeza Kavumbangu baada ya kufunga bao la pili |
|
Cannavaro anafunga bao la kwanza |
|
Kiiza na Kavumbangu wakimpongeza Cannavaro |
|
Chuji akimuelekeza Niyonzima namna ya kupiga mpira wa adhabu uliozaa bao la kwanza |
|
DUWA LA KUKU; Wachezaji wa JKT wakiomba dua kabla ya mechi |
|
Kikosi cha JKT leo |
|
Kavumbangu akishangilia bao la nne |
|
Makocha wa Yanga, Freddy Minziro (kulia) na Mfaume Athumani |
|
Mwenyekiti wa Yanga, akitoka kwenye chumba cha wachezaji wakati wa mapumziko |
|
Msuva anafanya safari |
|
Msuva hatari sana |
|
Shamte Ally anamtoka mtu |
|
Shamte anashughulika |
|
Wakubwa wakijipanga kwa kazi |
|
11 wa Yanga walioanza leo |
Na Mahmoud Zubeiry
YANGA SC jioni
hii imepata ushindi wa kwanza ndani ya mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, baada ya kuifunga JKT Ruvu mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Hadi
mapumziko Yanga walikuwa tayari mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na
Nahodha, Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’ dakika ya nne na Didier Kavumbangu
dakika ya 31, mabao yote yakitokana na kazi nzuri ya kiungo mshambuliaji Simon
Msuva.
Bao la
kwanza ulikuwa mpira wa adhabu uliopigwa na Haruna Niyonzima, baada ya Msuva
kuangushwa karibu kabisa na eneo la hatari la JKT Ruvu na bao la pili dogo huyo
aliyesajiliwa kutoka Moro United iliyoshuka daraja, alimpa pasi mshambuliaji wa
kimataifa wa Burundi, Kavumbangu.
Kipindi cha
pili, Yanga walirudi tena kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya
52, mfungaji Simon Msuva kabla ya Didier Kavumbangu kufunga la nne dakika ya 65.
JKT ilipata
bao lake la kufutia machozi dakika ya 68 mfungaji Credo Mwaipopo.
Katika mchezo
wa leo, Yanga ilicheza vizuri, wachezaji wakionana kwa pasi nzuri ndefu na
fupi, tofauti na ilivyokuwa kwenye iliyopita mjini Morogoro, ambako walifungwa
3-0 na Mtibwa Sugar.
Ikumbukwe mechi
ya kwanza, Yanga ililazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons mjini Mbeya.
Yanga leo
ilicheza chini ya kocha Msaidizi, Freddy Felix Minziro, baada ya aliyekuwa
Kocha Mkuu, Mbelgiji Tom Saintfiet kusitishiwa mkataba jana usiku, kufuatia kutofautiana
na uongozi.
Yanga SC; Yaw Berko, Mbuyu Twite, Oscar Joshua,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Nizar Khalfan/Shamte
Ally, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbangu/Jerry Tegete, Hamisi Kiiza na Simon
Msuva.
JKT; Said Mohamed, Kessy Mapande, Stanley
Nkomola, Damas Makwaya, Charles Timoth, Ally Khan, Haroun Adolf, Said Ahmed
‘Ortega’/Jimmy Shoji, Omar Changa/Furaha Tembo, Hussein Bunu na Sosstenes
Manyasi/Credo Mwaipopo.
Kwenye
Uwanja wa Chamazi, wenyeji Azam FC wameifunga Mtibwa Sugar 1-0, bao pekee la Kipre
Herman Tchetche, wakati Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha wenyeji JKT Oljoro 1-0
wameifunga Polisi Morogoro, bao pekee la Paul Ndonga dakika ya 13 na Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wenyeji Coastal
Union wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Toto Africans.
0 comments:
Post a Comment