Yanga SC |
Na Mahmoud Zubeiry
YANGA ya Dar
es Salaam, imekwama kuingia kambini leo Bagamoyo mkoani Pwani, kujiandaa na
mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wapinzani wao wa jadi,
Simba SC , Oktoba 3, mwaka huu na sasa zoezi hilo litafanyika kesho.
Wakati Yanga,
wakishindwa kuingia kambini leo, wapinzani wao wa jadi, Simba SC, tayari wapo
maeneo ya Mbweni, visiwani Zainzbar tangu saa 11:00 jioni wakijiandaa na mchezo
huo wa kukata na shoka, ambao utarushwa moja kwa moja na Televisheni ya Super
Sport.
Habari
kutoka ndani ya Yanga, zimesema kwamba timu hiyo itaingia kesho na itarudi Dar es Salaam Septemba 30, kucheza na African Lyon, na baada ya mechi itarejea huko kuendelea
kujiandaa na pambano la watani.
Mechi hiyo
inatarajiwa kuwa kali na ya kusisimua, kwa sababu mara ya mwisho timu hizo
zilipokutana, Yanga ilifungwa mabao 5-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kipigo hicho
ilidaiwa kilitokana na uongozi dhaifu chini ya Mwenyekiti, Wakili Lloyd
Baharagu Nchunga na pia ilikuwa sababu ya kumuondoa madarakani kiongozi huyo na
kufanyika uchaguzi mdogo, uliomuweka madarakani Yussuf Manji, Mwenyekiti mpya.
Tangu wakati
wa kampeni, miongoni mwa mambo ambayo wana Yanga wamekuwa wakiomba kutoka kwa
Manji ni kulipiwa kisasi cha 5-0, ingawa kwa hali ya sasa ya timu hizo, ubora
wao haupishani sana, hakuna hakika kama hilo litawezekana.
0 comments:
Post a Comment