// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); THOM ULIMWENGU SASA ATISHA MAZEMBE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE THOM ULIMWENGU SASA ATISHA MAZEMBE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, September 03, 2012

    THOM ULIMWENGU SASA ATISHA MAZEMBE

    Ulimwengu

    Na Prince Akbar
    THOMAS Emmanuel Ulimwengu, mshambuliaji chipukizi wa Tanzania, akicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika jana akitokea benchi kwenda kuchukua nafasi ya Kanda katika kikosi cha Tout Puissant Mazembe, alionyesha soka safi na kuitia misukosuko mno safu ya ulinzi ya Ahly, iliyolala 2-0.
    Katika mchezo huo, mshambuliaji mwingine Mtanzania, Mbwana Ally Samatta alifunga bao moja kwenye wa TP Mazembe mjini Lubumbashi, mechi ya Kundi B, Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Samatta alifunga bao hilo dakika ya 49, baada ya pasi nzuri ya Tressor Mabi Mputu, kabla ya D. Kanda kufunga la pili dakika ya 61, pasi ya Mputu tena. Thomas Ulimwengu aliingia dakika ya 67 kuchukua nafasi ya Kanda.
    Mbwana ni mchezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza cha Mazembe kwa mwaka wa pili sasa, lakini Ulimwengu alipandishwa kikosi hicho kwa mara ya kwanza mwezi uliopita, baada ya kukaa kikosi cha wachezaji wa akiba tangu asajiliwe katikati ya mwaka jana na jana amecheza mechi ya kwanza.
    Mazembe imefikisha pointi10 na kujihakikishia kutinga Nusu Fainali ya michuano hiyo, baada ya kucheza mechi tano, kushinda tatu, sare moja na Berekum Chelsea na kufungwa moja na Al Ahly ugenini,
    Al Ahly iliyotoa sare ya 1-1 na Berekum Chelsea nchini Ghana katika mechi yake iliyopita, ina pointi 10 pia, wakati wababe wapya wa Ghana wanashika nafasi ya tatu kwa pointi zao sita baada ya jana kutoka sare ya 1-1 na Zamalek, ambayo inashika mkia kwa pointi yake moja. 
    Sasa Ahly na TPM zitawania uongozi wa kundi hilo, ili kukwepa kukutana na Esperance ya Tunisia inayoongoza Kundi A. Katika mechi za mwisho za Kundi hilo, Ahly watamaliza na Zamalek mjini Cairo na Mazembe watamaliza na Berekum Chelsea nchini Ghana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: THOM ULIMWENGU SASA ATISHA MAZEMBE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top