Wachezaji wa Yanga wakishangilia 4-1 za JKT |
Na Mahmoud Zubeiry
SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF), limetoa ufafanuzi kuhusu kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, juu ya matumizi ya wachezaji wa kigeni na kusema kwamba Yanga
ilikuwa sahihi kutumia wachezaji wake wote watano katika mechi yao dhidi ya JKT
Ruvu, waliyoshinda mabao 4-1 juzi, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ofisa wa
Habari wa TFF, Boniphace Wambura ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba kanuni za sasa za
Ligi Kuu, zinairuhusu klabu kutumia wachezaji wote watano wa kigeni waliodhinishwa
kucheza ligi.
Mapema leo
kulikuwa kuna hofu kwa Yanga kupokonywa pointi tatu ilizovuna kutokana na
ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam kutokana na kuzidisha idadi ya wachezaji wa kigeni.
Mwenyekiti wa
Kamati ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Wallace Karia ni kama hajui vema
kanuni, baada ya kuiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, klabu inaruhusiwa
kusajili wachezaji watano wa kigeni, lakini itaruhusiwa kutumia watatu tu kwa
wakati mmoja.
Alisema mabadiliko
ya kanuni za wachezaji wa kigeni, kutoka watano hadi 10 kusajiliwa na watano
kucheza kwa wakati mmoja, yataanza kutumika msimu ujao.
“Tunatarajia
kukutana keshokutwa kupitia ripoti za mechi zote, ikiwemo mechi ambayo Emmanuel
Okwi alimpiga mchezaji mwenzake ngumi, baada ya kikao tutatoa ripoti ya
maamuzi,”alisema Karia.
Jumamosi,
Yanga ikimenyana na JKT Ruvu, Mgahan Yawe Berko, alianza langoni, Wanyarwanda
Mbuyu Twite alicheza beki ya kulia, Haruna Niyonzima alicheza kiungo cha juu,
Mrundi Didier Kavumbangu na Mganda Hamisi Kiiza walicheza mbele.
Kikosi cha
Yanga siku hiyo kilikuwa; Yaw Berko, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub
‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Nizar Khalfan/Shamte Ally,
Haruna Niyonzima, Didier Kavumbangu/Jerry Tegete, Hamisi Kiiza na Simon Msuva.
0 comments:
Post a Comment