Simba SC |
Na Dina Zubeiry
SIMBA SC leo inashuka kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
mjini Arusha kumenyana na City Stars ya Nairobi, katika mchezo wa kirafiki kujiandaa
na mechi ya Ngao ya jamii dhidi ya Azam FC, Septemba 11, mwaka huu, Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Hiyo itakuwa mechi ya pili kuzikutanisha timu hizo, awali Agosti
8, mwaka huu Simba ilichapwa mabao 3-1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Lakini
kufungwa huko kwa Simba kulitokana na kocha Mserbia Milovan Cirkovick, kubadilisha
karibu kikosi kizima kilichoanza na kuingiza wachezaji wapya, ambao waliitoa
City Stars ya Nairobi nyuma kwa 1-0 na kuipa ushindi wa 3-1.
Simba ilitangulia kupata bao kupitia kwa Felix Sunzu dakika
ya 15, pasi ya Mwinyi Kazimot na ilikwenda kupiumzika ikiwa mbele kwa bao hilo.
Lakini kipindi cha pili, kipa aliyempokea Juma Kaseja, Hamadi
Waziri alitunguliwa mabao matatu katika dakika 57 na Duncan Owiti, dakika ya 64
na Bruno Okullu na dakika ya 79 na Boniphace Onyango.
Tayari Simba imecheza mechi mbili Arusha, dhidi ya Mathare
United ya Kenya na JKT Oljoro ya Arusha, ambazo zote ilishinda 2-1,
mshambuliaji mpya Daniel Akuffo kutoka Ghana akifunga bao moja kila mechi,
Kiggi Makaasy na Mrisho Ngassa wakifunga mabao mengine.
Simba inajiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii Septemba 11, mwaka
huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambayo kihistoria hiyo itakuwa mechi ya
tano ya Ngao ya Jamii kuchezwa nchini na ya pili kukutanisha timu nje ya
wapinzani wa jadi wa soka ya Tanzania, Simba na Yanga.
Mtibwa ilicheza na Yanga mwaka 2009, baada ya Simba kugoma na
ikashinda mabao 2-1 na kutwaa Ngao, wakati kabla ya hapo, mwaka 2001, Ligi Kuu
ya Tanzania ikiwa bado inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia
bia ya Safari Lager, ilichezwa mechi ya kwanza ya Ngao kihistoria.
Katika mechi hiyo, Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Simba
na mwaka juzi Yanga iliifunga tena Simba kwa penali 3-1 kufuatia sare ya 0-0 na
mwaka jana, Simba ilitwaa Ngao ya kwanza katika historia yake, kwa kuifunga
Yanga mabao 2-0.
MABINGWA WA
MECHI ZA NGAO YA JAMII:
Mwaka Mshindi Matokeo
2001 Yanga 2-1 Simba
2010 Yanga
0-0 Simba (3-1penalti)
2011 Simba
2-0 Yanga
0 comments:
Post a Comment