// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC KIWANGO KINARIDHISHA, WAPINZANI WAJIPANGE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC KIWANGO KINARIDHISHA, WAPINZANI WAJIPANGE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, September 03, 2012

    SIMBA SC KIWANGO KINARIDHISHA, WAPINZANI WAJIPANGE

    Simba SC

    Na Prince Akbar
    KIWANGO cha Simba hivi sasa kipo vizuri na timu iko tayari kwa Ligi Kuu, tathmini inaonyesha. Pamoja na jana kulazimishwa sare ya 1-1 na Sony Sugar ya Kenya, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, lakini Simba ilicheza soka safi na washambuliaji wake walikosa mabao ya wazi zaidi ya matano.
    Lakini hata hali mbaya ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid katika eneo la kuchezea inachangia kupunguza idadi ya mabao kwa Simba.
    Katika mechi tatu ambazo Simba imecheza kwenye Uwanja huo, imevuna mabao matano na kufungwa matatu, na kikwazo kimekuwa kikionekana na hali ya eneo la kuchezea.
    Katika mchezo wa jana, bao la Simba lilifungwa na Daniel Akuffo, wakati Komabil Keita alijifunga katika jitihada za kuokoa na kuwapa Wakenya bao la kusawazisha.
    Awali, Simba ilicheza mechi mbili Arusha, dhidi ya Mathare United ya Kenya na JKT Oljoro ya Arusha, ambazo zote ilishinda 2-1, mshambuliaji mpya Daniel Akuffo kutoka Ghana akifunga bao moja kila mechi, Kiggi Makaasy na Mrisho Ngassa wakifunga mabao mengine.   
    Simba inajiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii Septemba 11, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambayo kihistoria hiyo itakuwa mechi ya tano ya Ngao ya Jamii kuchezwa nchini na ya pili kukutanisha timu nje ya wapinzani wa jadi wa soka ya Tanzania, Simba na Yanga.
    Mtibwa ilicheza na Yanga mwaka 2009, baada ya Simba kugoma na ikashinda mabao 2-1 na kutwaa Ngao, wakati kabla ya hapo, mwaka 2001, Ligi Kuu ya Tanzania ikiwa bado inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Safari Lager, ilichezwa mechi ya kwanza ya Ngao kihistoria.
    Katika mechi hiyo, Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Simba na mwaka juzi Yanga iliifunga tena Simba kwa penali 3-1 kufuatia sare ya 0-0 na mwaka jana, Simba ilitwaa Ngao ya kwanza katika historia yake, kwa kuifunga Yanga mabao 2-0. 

    MABINGWA WA MECHI ZA NGAO YA JAMII:
    Mwaka              Mshindi      Matokeo   
    2001                  Yanga         2-1 Simba
    2010                  Yanga         0-0 Simba (3-1penalti)
    2011                  Simba         2-0 Yanga
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC KIWANGO KINARIDHISHA, WAPINZANI WAJIPANGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top