|
Sunzu akimpongeza Edward na Kiemba baada ya kufunga bao la ushindi |
Na Mahmoud Zubeiry
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya soka ya Vodacom Tanzania
Bara, Simba SC leo wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuilaza mabao 2-1 Ruvu
Shooting ya Pwani, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Shukrani kwake mshambuliaji chipukizi, Christopher Edward
aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kwa
kufunga bao la ushindi dakika ya 80 na kuifanya Simba ifikishe pointi tisa baada
ya kucheza mechi tatu, nyavu zake zikitikiswa kwa mara ya kwanza leo.
Simba sasa inaendelea kuongoza Ligi Kuu, ikifuatiwa na Azam
yenye pointi saba, wakati watani wao wa jadi, Yanga wana pointi nne tu baada
ya mechi tatu.
Hadi mapumziko, Simba walikuwa tayari mbele kwa bao 1-0,
lililowekwa kimiani na mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu
Jr. dakika ya 29, akiunganisha krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’.
Katika dakika ya 45, kipa Benjamin Haule wa Ruvu Shooting
alipangua mkwaju wa penalti wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana, Daniel
Akuffor baada ya beki mmoja wa timu hiyo kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Kipindi cha pili, Ruvu Shooting inayofundishwa na kocha
maarufu nchnini, Charles Boniface Mkwasa ilisawazisha bao dakika ya 80, baada
ya Seif Rashid kutumia vizuri makosa ya beki Juma Nyosso dakika ya 75.
Seif aliupitia mpira miguuni mwa Nyosso, ambaye alianzishiwa
na kipa Juma Kaseja na kutokana na kuchelewa kuamua, akasababisha kilichotokea.
Shukrani wake, chipukizi Edward aliyeifungia bao la ushindi Simba
inayofundishwa na Mserbia, Milovan Cirkovick dakika ya 80.
Simba SC; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah,
Shomari Kapombe, Juma Nyosso, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Ramadhani Chombo
‘Redondo’/Edward, Felix Sunzu, Daniel Akuffo/Boban na Mrisho Ngassa.
Ruvu
Shooting; Benjamin Haule, Michael Pius, Mau Bofu, George
Michael, Said Suzan, Gideon David, Abdulrahman Mussa, Hassan Dilunga, Paul
Ndauka/Seif rashid, Hussein Said na Said Dilunga.
|
Kikosi cha Simba leo |
|
Manahodha Benjamin Haule wa Ruvu na Juma Kaseja wa Simba wakisalimiana kabla ya mechi |
|
Hatari kwenye lango la Simba |
|
Beki MIchael Pius wa Ruvu akiwatoka kiungo Amri Kiemba na beki Amir Maftah wa Simba |
|
Kiemba akimdhibiti Abdulrahman Mussa, huku Kapombe akiwa tayari kutoa msaada |
|
Kiungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto akiokoa |
|
Kapombe akimdhibiti Hussein Said wa Ruvu |
|
Kiemba akimkabili Hussein Said |
|
Kiemba akiondosha mpira miguuni mwa Hussein Said |
|
Maftah akimdhibiti Said Dilunga |
|
Benja Haule akipangua penalti ya Akuffo |
|
Kocha wa Ruvu, Mkwasa akilalamika kwa refa wa akiba, Oden Mbaga kuhusu marefa wa mechi ya leo |
|
Mau Boffu akiondosha mpira miguuni kwa Akuffo |
|
Chollo akiwatoka Mau Bofu na Abdulrahman Mussa |
|
Akuffo anatia krosi |
|
Mrisho Ngassa anaambaa |
|
Benja Haule akidaka mpira mbele ya Ngassa, huku akilindwa na mabeki wake |
|
Ngassa a napaa |
|
Benja akidaka mbele ya Sunzu |
|
Kikosi cha Ruvu Shooting leo |
0 comments:
Post a Comment