Jakob Michelsen, kocha wa timu za vijana |
Na Princess Asia
TIMU
ya soka ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys
iliyokuwa kambini kujiandaa kwa mechi dhidi ya Kenya itavunja rasmi kambi yake leo
kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Ashanti United.
Mechi
hiyo dhidi ya Ashanti United iliyoko daraja la kwanza itachezwa kuanzia saa 10
jioni Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kwa kiingilio cha sh.
2,000.
Serengeti
Boys ilikuwa icheze Septemba 9 mwaka huu na Kenya kwenye mechi ya raundi ya
kwanza ya michuano ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, lakini Kenya
ikajitoa ambapo sasa itacheza na Misri katika raundi ya pili. Mechi ya kwanza
itachezwa Oktoba 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Mwishoni
mwa Septemba, Serengeti Boys itarejea tena kambini kujiandaa kuikabili Misri
ambapo kabla inatarajia kupata mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu
itakayotangazwa baadaye.
0 comments:
Post a Comment