Cristiano Ronaldo anaweza kuwa tayari kumuumiza kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho kwa kuihama klabu hiyo.
Taarifa nchini Hispania zinasema mshambuliaji huyo Mreno amemuambia rais wa klabu hiyo, Florentino Perez kwamba anataka kuondoka kwa mabingwa hao wa Hispania.
Imeripotiwa kwa mapana marefu kwamba, Ronaldo alikuwa na kikao Jumamosi na Perez, Mkurugenzi Mkuu, Jose Angel Sanchez na wakala wake, Jorge Mendes.
Cristiano Ronaldo akitoka baada ya kuumia
Redio nchini Hispania imesema kwamba Ronaldo, ambaye alifunga mabao 46 kwenye ligi msimu uliopita, hapatani na baadhi ya wachezaji kwenye klabu hiyo na hajisikii kama anapewa thamani ya juu na klabu hiyo.
Vyanzo vingine vinasema kwamba, nyota huyo - licha ya kuwa amebakiza miaka mitatu katika mkataba wake - hafurahii kuona hajapewa ofa ya mkataba mpya.
Ronaldo aling'ara Jumapili ya jana katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Granada, akifunga mabao mawili.
Lakini mkali huyo mwenye umri wa miaka 27, alitolewa na Mourinho baada ya kupigwa kwanja la nguvu na Borja Gomez wa Granada kipinfi cha pili.
Ronaldo aliuamia hapa na akatolewa jana
Hivi tu, kuwapungia mikono mashabiki ilitosha kwa Ronaldo baada ya kufunga jana
Wasiwasi ndani ya Madrid unaletwa na kitendo cha mchezaji huyo kutoshangilia mabao.
Baada ya mechi, mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United, alisema; 'Nina machungu - ninapokuwa sishangilii mabao maana yake sina furaha. 'Ni kitu ch kawaida katika mchezo. Real Madrid wanajua kwa nini sina furaha.’
Nahodha huyo wa Ureno anashindwa kushangilia na wenzake kwa sababu hana furaha.
Ronaldo, alianzia soka katika klabu ya Sporting Lisbon ya kwao, kabla ya kutimkia Manchester United ambayo ilimuuza kwa dau la pauni Milioni 82 mwaka 2009.
Mchezaji mwenzake wa zamani wa United, Gary Neville alizungumzia habari hiyo kwa mzaha akisema Ronaldo anakumbuka 'mavituz' ya Kiingereza.
Aliandika kwenye twita: 'Cristiano ana machungu RM anasema. Sina uhakika kama amewahi kuwa na furaha huko. ( maneno yangu si makini). nilimuambia ataikumbuka Jam Roly!!'
Ronaldo asiye na furaha baafa ya kutolewa mechi ya jana
Read more: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2197510/Cristiano-Ronaldo-leave-Real-Madrid.html#ixzz25PUnHya7
0 comments:
Post a Comment