Okwi |
Na Mahmoud Zubeiry
MSHAMBULIAJI wa Simba SC, Mganda, Emmanuel Okwi hatacheza mechi dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga, Oktoba 3, mwaka huu baada ya kikao cha Kamati ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, chini ya Mwenyekiti wake, Wallace Karia juzi jana kumfungia mechi tatu na kumtoza faini ya Sh. 300,000 kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa JKT Ruvu, Kessy Mapande.
Okwi alifanya hivyo J akilipa kisasi cha kuchezewa rafu Jumatano iliyopita, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Tayari Okwi amekosa mechi moja ya juzi dhidi ya Ruvu Shooting na wakati, na sasa atakosa mechi mbili zaidi, dhidi ya Prisons na dhidi ya Yanga na baada ya hapo atakuwa huru kuendelea kumtukia mwajiri wake.
Siyo siri, kuelekea pambano la watani wa jadi, Okwi alikuwa ni homa kwa Yanga, hasa wakikumbuka namna alivyowanyanyasa katika mechi iliyopita, akifunga mabao mawili kwenye ushindi wa 5-0 na kusababisha mawili.
Tayari Simba SC ipo kambini maeneo ya Mbweni, Zanzibar ikijiandaa na pambano hilo la Oktoba 3, mwaka huu, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam tangu jana jioni.
Simba SC jana ilifanya mazoezi katika ufukwe wa Coco Beach, Dar es Salaam asubuhi kabla ya kupanda boti jioni kwenda kisiwani humo kwa maandalizi ya kuendeleza ‘mila’ ya kuwanyanyasa wapinzani wao jadi, Yanga.
Wekundu hao wa Msimbazi watapanda boti kurejea Dar es Salaam mara moja Jumamosi kucheza na Prisons na baada ya hapo, watapanda tena boti kurejea visiwani humo kuendelea na maandalizi yao.
0 comments:
Post a Comment