Nsa Job anayebinuka tik tak mbele ya Juma Nyosso wa Simba wakati akiwa Yanga |
Na Princess Asia
NSA Job
amesema safari ya kukimbilia kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara ilianza rasmi jana Uwanja wa Mkwakwani, Tanga baada ya kufunga mabao
mawili katika ushindi wa 3-2 wa Coastal Union dhidi ya Kagera Sugar.
“Ndio
nimeanza, nataka kuwa mfungaji bora msimu huu, hesabu zimeanza sasa, wapenzi na
mashabiki wa Coastal watarajie mabao zaidi,”alisema jana alipozungumza na BIN
ZUBEIRY kwa simu kutoka Tanga.
Coastal Union
jana ilipaa hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi, kufuatia 3-2 dhidi ya
Kagera Sugar ya Bukoba, kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, katika mchezo
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ikifungana kwa kila kitu na Azam FC.
Ushindi huo,
ulitokana na mabao ya Daniel Lyanga na Nsa Job mawili, ni wa pili katika mechi
nne za Wagosi wa Kaya tangu kuanza kwa Ligi Kuu, unakuja siku moja baada ya
kujiuzulu kwa aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Juma Mgunda.
Mgunda,
alijiuzulu jana akisema ameamua kufanya hivyo mapema, kabla ya mambo
hayajaribika, ili mwalimu mpya anayekuja afanye kazi vizuri.
Akizungumza
na BIN ZUBEIRY juzi, Mgunda alisema
kwamba anaachia timu baada ya kucheza mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, akiwa ameshinda moja na kutoa sare mbili.
“Kama
utaweza kuona naiacha timu ikiwa kwenye hali nzuri kuliko Yanga, ambao wamefungwa
mechi moja, sare moja na kushinda moja, naondoka kwa moyo mkunjufu, sina
kinyongo na mtu,”alisema.
Mgunda
alisema hiyo ndio hulka yake tangu anacheza Coastal Union, kuwa na moyo swafi
na ataendelea kuwa hivyo. “Mimi ni mpenzi wa Coastal Union, hakuna asiyejua, na
kwa manufaa ya timu, naondoka,”alisema.
Kumekuwa
kama kuna kampeni ya kumvuruga Mgunda kazini ambayo imekuwa ikiendeshwa kwenye
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kwa kumzomea kila timu inapocheza, hatimaye ameamua
kuwaachia timu.
Kwa sasa
Coastal, imebaki na kocha Msaidizi, Habib Kondo ambaye msimu uliopita alikuwa
kocha wa Villa Squad ya Kinondoni, iliyoshuka daraja na jana ndio aliiongoza
timu hiyo ya Barabara ya 13, katika mechi na Kagera Sugar.
Mgunda
anakuwa kocha wa pili wa Ligi Kuu kuachia timu, baada ya Mbelgiiji, Tom
Sainftiet ambaye amefukuzwa Yanga, baada ya kutofautiana na uongozi, akiwa
ameiongoza timu kwenye mechi mbili tu za Ligi Kuu, akitoa sare moja na kufungwa
moja. Hemed Morocco, kocha wa Mafunzo ya Zanzibar yupo kwenye mazungumzo na
uongozi wa Coastal Union ya Tanga, ili awe kocha mpya wa timu hiyo kufuatia
kubwagwa manyanga kwa Mgunda.
Katika mechi
nyingine ya ligi hiyo, Polisi Morogoro imelazimishwa sare na Toto African ya
Mwanza kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro jioni hii.
0 comments:
Post a Comment