Shujaa wa leo Nizar |
Na Prince Akbar
YANGA
imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya African Lyon katika mchezo wa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Shukrani kwake
kiungo anayecheza kwa nadra kwenye timu hiyo, Nizar Khalfan aliyefunga mabao ya
ushindi dakika ya 65 na 88, akitokea benchi kuchukua nafasi ya Frank Domayo.
Nizar alifunga
bao la pili, sekunde chache baada ya Benedictor Mwamlangala kuisawazishia African
Lyon bao lililodumu tangu dakika ya 17, baada ya Nahodha wa Yanga, kutangulia
kufunga dakika ya 17.
Ushindi huo,
unaifanya Yanga ifikishe pointi saba, baada ya kucheza mechi nne na kupanda
hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, ikiwa inalingana na Coastal kwa pointi
na wastani wa mabao, ingawa Coastal wako nyuma kwa mechi moja.
Simba bado
inaongoza ligi hiyo, kwa pointi zake 12, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 10.
Yanga SC; Ally Mustapha 'Barthez', Mbuyu Twite,
Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub 'Cannavaro', Athumani Iddi 'Chuji', Simon Msuva, Frank Domayo/Nizar Khalfan, Didier Kavumbagu, Hamisi
Kiiza/Said Bahanuzi na Haruna Niyonzima.
MSIMAMO WA LIGI KUU BARA
P W D L GF GA GD P
Simba SC 4 4 - - 9 2 7 12
Azam FC 4 3 1 - 6 1 5 10
Coastal 3 2 1 - 5 3 2 7
Yanga SC 4 2 1 1 7 5 2 7
Prisons 4 1 2 1 4 4 - 5
JKT Oljoro 3 1 2 1 2 1 1 5
Mtibwa Sugar 3 1 1 1 3 1 2 4
Toto African 3 - 3 1 3 2 1 3
Ruvu Shooting 3 1 - 2 4 5 -1 3
African Lyon 4 1 - 3 3 8 -5 3
JKT Ruvu 4 1 - 3 3 10 -7 3
Polisi Moro 3 - 2 1 - 1 -1 2
Kagera Sugar 3 - 1 2 2 4 -2 1
JKT Mgambo 3 - - 3 1 3 -2 0
0 comments:
Post a Comment