Mgunda kulia akiwa na Kondo kushoto |
Na Mahmoud Zubeiry
JUMA Mgunda,
kocha wa Cosatal Union ya Tanga amesema ameamua kujiuzulu mapema, kabla ya
mambo hayajaribika, ili mwalimu mpya anayekuja afanye kazi vizuri.
Akizungumza na
BIN
ZUBEIRY jioni hii, Mgunda amesema kwamba anaachia timu baada ya kucheza
mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, akiwa ameshinda moja na kutoa
sare mbili.
“Kama utaweza
kuona naiacha timu ikiwa kwenye hali nzuri kuliko Yanga, ambao wamefungwa mechi
moja, sare moja na kushinda moja, naondoka kwa moyo mkunjufu, sina kinyongo na
mtu,”alisema.
Mgunda amesema
hiyo ndio hulka yake tangu anacheza Coastal Union, kuwa na moyo swafi na
ataendelea kuwa hivyo. “Mimi ni mpenzi wa Coastal Union, hakuna asiyejua, na
kwa manufaa ya timu, naondoka,”alisema.
Kumekuwa kama
kuna kampeni ya kumvuruga Mgunda kazini ambayo imekuwa ikiendeshwa kwenye Uwanja
wa Mkwakwani, Tanga kwa kumzomea kila timu inapocheza, hatimaye ameamua
kuwaachia timu.
Sasa Coastal,
inabaki chini ya kocha Msaidizi, Habib Kondo ambaye msimu uliopita alikuwa
kocha wa Villa Squad ya Kinondoni, iliyoshuka daraja.
Mgunda anakuwa
kocha wa pili wa Ligi Kuu kuachia timu, baada ya Mbelgiiji, Tom Sainftiet
ambaye amefukuzwa Yanga, baada ya kutofautiana na uongozi, akiwa ameiongoza
timu kwenye mechi mbili tu za Ligi Kuu, akitoa sare moja na kufungwa moja.
0 comments:
Post a Comment