Na Mahmoud Zubeiry
SIMBA SC
inaendelea vizuri na maandalizi yake ya pambano dhidi ya watani wao wa jadi,
Yanga SC, Oktoba 3, mwaka huu, ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Kiislam,
Kwerekwe, visiwani Zanzibar na kambi yao ipo Chukwani.
Morali ya
kambi ipo juu na wachezaji wote wako fiti, wakijifua kwa shauku kubwa ili
kumvutia kocha Mserbia, Milovan Cirkovick awape nafasi ya kucheza Oktoba 3,
kuanzia sa 1:00 usiku.
Simba
itarejea Dar es Salaam Jumamosi kucheza mechi na Prisons ya Mbeya Uwanja wa
Taifa, kisha kurejea tena visiwani humo kuendelea na maandalizi ya mchezo wa
Jumamosi ijayo.
Hata hivyo,
katika michezo miwili ijayo, Simba itamkosa mshambuliaji wake Mganda, Emmanuel
Okwi ambaye amefungiwa na Kamati ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, chini ya
Mwenyekiti wake, Wallace Karia kufuatia kikao cha juzi, sambamba kumtoza faini
ya Sh. 500,000 kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa JKT Ruvu, Kessy Mapande.
Okwi
alifanya hivyo akilipa kisasi cha kuchezewa rafu Jumatano iliyopita, Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Tayari Okwi
amekosa mechi moja ya juzi dhidi ya Ruvu Shooting na wakati, na sasa atakosa mechi
mbili zaidi, dhidi ya Prisons na dhidi ya Yanga na baada ya hapo atakuwa huru
kuendelea kumtukia mwajiri wake.
Siyo siri,
kuelekea pambano la watani wa jadi, Okwi alikuwa ni homa kwa Yanga, hasa
wakikumbuka namna alivyowanyanyasa katika mechi iliyopita, akifunga mabao
mawili kwenye ushindi wa 5-0 na kusababisha mawili.
0 comments:
Post a Comment