Mmoja wa viongozi wa Matawi ya Yanga, Said Motisha akizungumza kwenye Mkutano huo leo |
Wanachama wakipongezana baada ya Mkutano |
Na Emmanuel Ndege
KATIKA
kuhakikisha mnyama hatoki Oktoba 3, mwaka huu- Matawi ya Yanga yamekutana leo
katika kikao maalum kujadili namna ya kuifunga Simba siku hiyo, Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Kikao kilichodumu
kwa takriban saa mbili, kilifanyika makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga
na Jangwani.
Ajenda kuu,
ilikuwa ni kuua mnyama na watu wakagawana majukumu kwa makubaliano kazi inaanza
mara moja.
Wakati huo
huo, kikosi cha Yanga kimeingia kambini leo katika hoteli ya Uplands,
Changanyikeni, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo huo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wapinzani wao hao wa jadi.
Awali, Yanga
ilipanga kwenda kuweka kambi wilayani Bagamoyo mkoani Pwani jana, lakini
maamuzi yamebadilika.
Wakati
Yanga, wanaingia kambini leo Changanyikeni, wapinzani wao wa jadi, Simba SC,
tayari wapo visiwani Zainzbar tangu juzi saa 11:00 jioni wakijiandaa na mchezo
huo wa kukata na shoka, ambao utarushwa moja kwa moja na Televisheni ya Super
Sport, kuanzia saa 1:00 usiku.
Kabla ya
kucheza na Simba, Yanga Jumapili itacheza na African Lyon, Uwanja wa Taifa.
Mechi hiyo
inatarajiwa kuwa kali na ya kusisimua, kwa sababu mara ya mwisho timu hizo
zilipokutana, Yanga ilifungwa mabao 5-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kipigo hicho
ilidaiwa kilitokana na uongozi dhaifu chini ya Mwenyekiti, Wakili Lloyd
Baharagu Nchunga na pia ilikuwa sababu ya kumuondoa madarakani kiongozi huyo na
kufanyika uchaguzi mdogo, uliomuweka madarakani Yussuf Manji, Mwenyekiti mpya.
Tangu wakati
wa kampeni, miongoni mwa mambo ambayo wana Yanga wamekuwa wakiomba kutoka kwa
Manji ni kulipiwa kisasi cha 5-0, ingawa kwa hali ya sasa ya timu hizo, ubora
wao haupishani sana, hakuna hakika kama hilo litawezekana.
0 comments:
Post a Comment