Israel Mujuni Nkongo, mmoja wa marefa wa FIFA |
Na
Mahmoud Zubeiry
KWA
sasa Tanzania ina marefa watano tu wanaotambuliwa na Shirikisho la Soka la
Kimataifa (FIFA), kati yao mmoja mwanamke mmoja tu, Judith Gamba kutoka Arusha.
Marefa
wa kiume ni Isarel Mujuni Nkongo (Dar es Salaam), Charles Orden Mbaga (Dar es
Salaam), Waziri Shekha (Z’bar) na Ramadhani Kibo (Z’bar).
Aidha,
marefa wasaidizi, maarufu kama washika vibendera wanaotambuliwa na FIFA ni 10,
kati yao wawili wanawake, ambao ni Sada Tibabimale (Mwanza) na Mwanahija Makame
(Z’bar), wakati wanaume ni Hamisi Chang’walu (Dar es Salaam), John Kanyenye (Mbeya)
Jesse
Rasmo (Morogoro), Samuel Mpenzu (Arusha), Ferdinand Chacha (Kagera), Hamisi Maswa
(Z’bar), Josephat Bulari (Z’bar) na Ramadhan Chinduli (Z’bar).
Marefa
hawa ambao huchezesha mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua za awali za Kombe
la Mataifa ya Afrika na Kombe la Dunia, ndio kati yao wanapewa nafasi ya
kuchezesha mechi za watani wa jadi, Simba na Yanga.
Lakini
mechi ya mwisho ya Ligi Kuu msimu uliopita baina ya wapinzani hao wa jadi,
ambayo Yanga ilifungwa 5-0, haikuchezeshwa na marefa wa FIFA, ambao ni Hashim
Abadallah aliyesaidiwa na Iddi Maganga na Omar Kambangwa, wote wa Dar es
Salaam.
Kabla
ya hapo, kwa muda mrefu, mechi hizo za watani zimekuwa zikichezeshwa na Orden
Mbaga na Israel Nkongo- baada ya utawala wa Victor Mwandike, Paschal Chiganga
na Emmanuel Chaula, ambao waliwapokea Omar Abdulkadir, Nassor Hamdoun na Kanali Issaro Chacha.
0 comments:
Post a Comment