Tetesi za Jumatatu magazeti Ulaya
LIVERPOOL KUMSAJILI MICHAEL OWEN KUMALIZA UKAME WA MABAO ANFIELD
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers anaweza kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Wekundu hao, Michael Owen baada ya kushuhudia ubutu wa safu yake ya ushambuliaji, wakati wakichapwa mabao 2-0 na Arsenal Uwanja wa Anfield jana.
Sunderland pia imewasiliana na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32, Owen, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru, baada ya kutemwa na Manchester United mwishoni mwa msimu.
Kocha wa Swansea, Michael Laudrup amesema kwamba atalazimika kuingia sokoni kununua mchezaji wa kuziba pengo la beki wa kushoto, Neil Taylor, ambaye ameumia kifundo cha mguu katika mechi ya Jumamosi ya sare ya 2-2 na Sunderland na anatarajiwa kuwa nje ya Uwanja msimu mzima.
Raul Meireles anaweza kuondoka Chelsea baada ya Fenerbahce kuonyesha nia ya dhati ya kumsajili kiungo huyo Mreno mwenye umri wa miaka 29.
Tottenham iko tayari kuwaruhusu makipa Carlo Cudicini, mwenye umri wa miaka 38, na Heurelho Gomes mwenye miaka 31 kwenda klabu za Daraja la Kwanza kwa mkopo, baada ya wawili hao kupoteza namba mbele ya kipa Mfaransa, Hugo Lloris mwenye umri wa miaka 25 kutoka Lyon.
OTHER GOSSIP
Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Robbie Fowler amesema kwamba ameshangazwa na kitendo cha Wekundu hao kumruhusu mshambuliaji Andy Carroll kuhamia West Ham.
ARSENAL IKASAKE MATAJI KWENYE WAVU
Arsenal haijashinda taji lolote kwa zaidi ya miaka saba na klabu hiyo imeambiwa iwapeleke baadhi ya wachezaji wake kwenye mchezo mpya, mpira wa wavu ili kumaliza ukame wa mataji.
Fulham inaweza kumuuza Mousa Dembele kwa Tottenham katika dirisha dogo, lakini mashabiki wa Cottagersmuda si mrefu wataendelea kuimba jina la mchezaji huyo tena, baada ya mmoja wa wachezaji wake wa akademi, ambaye pia anaitwa Mousa Dembele - kufunga hat-trick katika timu ya U18 ya klabu hiyo, dhidi ya Crystal Palace.
0 comments:
Post a Comment