Washiriki wa kliniki ya Airtel Rising Stars wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumalizika kliniki hiyo ambayo ilikuwa inafanyika Nairobi, Kenya.
|
Prince
Akbar, Nairobi
KLINIKI ya Airtel Rising Stars imefikia mwisho,
Nairobi nchini Kenya. Kliniki hiyo ambayo ilizinduliwa Jumatatu ya tarehe 27
Agosti ilihudhuriwa na vijana zaidi ya 50 kutoka barani Afrika. Washiriki wa
kliniki hiyo wametumia muda wa wiki moja kupata mafunzo kutoka kwa waalimu wa
soka ya vijana kutoka Klabu ya Manchester United. Vijana walihudhuria kliniki
hiyo walichanguliwa kutokana na kufanya vyema kwenye michuano ya Airtel Rising
Stars Pan-Afrika, michuano yenye lengo la kutafuta na kukuza vipaji vya soka.
Mpango wa Airtel Rising Stars – ambao umeingia mwaka
wa pili – imetajwa kuwa moja ya michuano mikubwa barani Afrika, huku timu
18,000, wachezaji 324,000 kutoka nchi 15 za Afrika zikishiriki kwa mwaka huu.
Pia, imekuwa ni michuano ya kipekee kwa kushirikisha wasichana.
Akiongelea kuhusu kliniki hiyo, Ofisa Masoko Mkuu wa
Airtel Afrika, Andre Beyers anasema, ‘Kwa mara nyingine mafanikio ya kliniki ya
mwaka huu imeonyesha jinsi soka inaweza kuunganisha jamii na makabila yote
pamoja. Na kuongeza michuano ya Pan-Afrika ambayo imeleta vijana kutoka maeneo
mbali mbali barani Afrika, kuzoena na kubadilishana maadili ya kila mmoja, kwa
hakika ni hatua moja kubwa kwa maisha ya kila mmoja’.
Kwenye sherehe za ufungaji wa kliniki hiyo, kila
mshiriki alipokea medali ya ushiriki ambayo ilitolewa kulingana na hadhi ya
Klabu ya Manchester United. Wakati wa kliniki hiyo, vijana wameweza kujifunza
mambo mbali mbali kama – ukabaji, kufunga, kuzuia na hata mbinu zingine za
kijanja za soka – na kushauriwa kuzitumia kila wanapokuwa uwanjani.
Klikini hiyo ni mpango wa miaka mine wa ushirikiano
baina ya Manchester United na Airtel Afrika kwa shule za soka za vijana ya
Manchester United kutoa mafunzo kwa vijana chipukizi. Shule za soka za vijana
za Manchester United zimekuwepo kwa miaka 12 sasa na utoa mafunzo kama haya kwa
wanafunzi zaidi ya 120,000 duniani kila mwaka.
0 comments:
Post a Comment