Didier Kavumbangu; Mechi nne hakuna bao |
Na
Mahmoud Zubeiry
MSHAMBULIAJI
mpya wa Yanga, Didier Kavumbangu bado anasota kuonyesha makali yake katika
klabu yake mpya, Yanga iliyomsajili mwezi uliopita kutoka Atletico ya Burundi.
Kwa
mara nyingine jana mpachika mabao huyo wa kimataifa wa Burundi alicheza mechi
ya nne akiwa na jezi ya Yanga na kumaliza dakika 90 bila bao.
Yanga
jana ilishinda 2-1, kwa mabao ya mawili ya dakika za lala salama, dhidi ya
Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Saidi
Bahanuzi ‘Spider Man’, kwa mara nyingine jana alikuwa shujaa wa Yanga baada ya
kufunga bao la ushindi dakika ya 85 katika mchezo, ambao Coastal Union
ilimpoteza kiungo wake Jerry Santo aliyepewa kadi nyekundu kwa kumtolea maneno
machafu refa Hashim Abdallah dakika ya 59.
Hilo
lilikua bao lake la nane Bahanuzi tangu aanze kuichezea Yanga miezi miwili
iliyopita, akitokea Mtibwa Sugar. Awali ya hapo, beki Mganda, Philip Kaira
alijifunga katika harakati za kuokoa krosi ya Shamte Ally dakika ya 84.
Hadi
mapumziko, Coastal tayari walikuwa mbele kwa bao hilo moja lililotiwa kimiani
na kiungo Razack Khalfan, aliyefumua shuti la umbali wa mita 26.
Razack
alitokea Yanga B mwaka 2008 na kupandishwa kikosi cha kwanza mwaka 2009, chini
ya kocha Mserbia, Profesa Dusan Savo Kondic, lakini misimu miwili baadaye
akatolewa kwa mkopo African Lyon, ambao umeisha na msimu huu amesaini Coastal.
Kwa
ujumla Razack, mdogo wa kiungo wa Yanga, Nizar Khalfan alicheza soka ya
kusababisha swali kwa nini Yanga ilimuacha.
Mechi
hiyo ilichezeshwa na refa Hashim Abdallah aliyechezesha pia mechi ambayo Yanga
ililala 5-0 kwa Simba katika Ligi Kuu msimu uliopita, ambaye leo amesaidiwa na
Shaffi Mohamed na Iddi Maganga.
Kocha wa Yanga alipowasili Uwanja wa ndege miezi miwili iliyopita, hapa anapokewa na viongozi wa timu hiyo. |
Awali,
mchezo huo nusura uvunjike, baada ya kocha wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet
kutoa timu uwanjani kutokana na kucheleweshwa kwa muda wa kuanza, ambao
kimakubaliano ulikuwa saa 10:00 jioni.
Lakini
Coastal walichelewa kufika uwanjani (walifika saa 10:05 jioni ) na kuanza
kwanza kupasha misuli moto, jambo ambalo lilimkera Saintfiet na kusistiza
waachane na mazoezi yao mechi ianze, lakini makocha wa timu hiyo ya Tanga, Juma
Mgunda na Habib Kondo waliendelea na biashara yao.
Saintfiet
akatoa timu yake uwanjani, kabla ya kwenda kubembelezwa na viongozi wake, ndipo
akarejesha timu na mpira ukaanza saa 10:31 jioni.
Kwa
ujumloa Coastal walitawala kipindi cha kwanza mchezo huo na kipindi cha pili
japokuwa mchezo ulikuwa wa pande zote mbili hata baada ya Santo kutolewa kwa
kadi nyekundu, lakini Yanga waliuteka kabisa dakika 15 za mwishoni.
Kwa
Coastal, hiyo inakuwa mechi ya nne Coastal wanafungwa ndani ya mechi tano za
kujipima nguvu, nyingine zikiwa dhidi ya Bandari mara mbili, 3-2 Mombasa na 2-0
Tanga na 2-1 dhidi ya Polisi mjini Morogoro, wakati mechi waliyoshinda ni dhidi
ya JKT Oljoro 2-0.
Kwa
Yanga, chini ya kocha wake Mbelgiji, Saintfiet, hiyo inakuwa mechi ya 10
anashinda kati ya 11 alizocheza tangu ajiunge na kabu hiyo miezi miwili
iliyopita.
Kocha
Saintfiet alimpumzisha dakika ya 75 Kavumbangu na kumuingiza Jerry Tegete,
ambaye naye pia hakuziona nyavu.
Mechi
alizoichezea Yanga Kavumbangu ni dhidi ya African Lyon, Yanga ikishinda 4-0 Dar
es Salaam, Rayon mjini Kigali, Rwanda ambayo timu hiyo ilishinda 2-0 na dhidi
ya Polisi nchini humo pia, ambayo timu hiyo ilishinda 2-1.
Yanga
ilivutiwa na mshambuliaji huyo na kumsajili, kwa sababu aliwafunga mabao mawili
katika mchezo wa kwanza wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la
Kagame, ikilala 2-0 dhidi ya Atletico katika michuano ambayo mwisho wa simu
timu hiyo iliibuka bingwa.
Kwa
upande wake, kocha Saintfiet ameendeleza rekodi yake nzuri akishinda mechi ya
10 kati ya 11 alizoiongoza timu hiyo tangu ajiunge nayo miezi miwili iliyopita.
REKODI
YA SAINTFIET YANGA
1.
Yanga Vs JKT Ruvu 2-0
2.
Yanga Vs Atletico (Burundi) 0-2
3.
Yanga Vs Waw Salam (Sudan Kusini) 7-1
4.
Yanga Vs APR (Rwanda) 2-0
5.
Yanga Vs Mafunzo (Z’bar) 1-1
(5-3penalti)
6.
Yanga Vs APR (Rwanda) 1-0
7.
Yanga Vs Azam 2-0
8.
Yanga Vs African Lyon 4-0
9.
Yanga Vs Rayon (Rwanda) 2-0
10. Yanga Vs Polisi (Rwanda) 2-1
11.
Yanga Vs Coastal Union 2-1
0 comments:
Post a Comment