Mgongolwa |
Na
Mahmoud Zubeiry
KAMATI
ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini
ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa, kesho saa 6:00 mchana itakukutana itakutana
na klabu zilizoweka na zilizowekewa pingamizi za usajili wa wachezaji kwa
ujumla kuelekea msimu wa Ligi Kuu ya Bara 2012/2013.
Habari
za ndani kutoka TFF, ambazo BIN ZUBEIRY imezipata, zimesema
kwamba, viongozi tu wa klabu zilizoweka na kuwekewa pingamizi, ndio watakaohudhuria
kikao cha kesho, makao makuu ya TFF, Uwanja wa Karume, Ilala mjini Dar es
Salaam.
Hatua
hiyo inafuatia kikao cha Kamati ya Mgongolwa tangu jana asubuhi hadi usiku,
kumalizika bila kupata suluhisho la pingamizi hizo na sasa inaamua kutumia
busara ya kuzikutanisha pande zinazopingana kujaribu kupata suluhu.
Katika
pingamizi hizo, Azam inapinga usajili wa Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kwenda Simba
kwa maelezo bado ina mkataba naye unaomalizika Juni 11 mwakani na ili kumuachia
kiungo huyo iliyemsajili kutoka Simba miaka mitatu iliyopoita, inataka dola za
Kimarekani 50,000 ingawa Simba wamefika dola 20,000 ambazo pia wameomba kulipa
kwa awamu.
Habari
zaidi zinasema kwamba, Simba nayo inataka dola 60,000 kutoka kwa Yanga, ili
wawauzie beki Kevin Yondan. Simba imepinga Yondan kusajiliwa Yanga kwa maelezo
kuwa ina mkataba naye uliosainiwa Desemba 23 mwaka jana.
Vilevile
Simba imewasilisha malalamiko ya mchezo usio wa kiungwana katika usajili wa
Mbuyu Twite aliyeko Yanga kwa maelezo alisaini mkataba na klabu yao Agosti Mosi
mwaka huu mbele yao, viongozi wa Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) na APR
ambapo alilipwa dola 30,000 na nyingine 2,000 ikiwa ni fedha ya kujikimu na
nauli yake ya kujiunga na klabu hiyo.
Nayo
Yanga inapinga Simba kuwaacha wachezaji Dan Mrwanda, Haruna Shamte, Kanu
Mbiyavanga na Lino Masombo kwa maelezo walishapatiwa leseni za kucheza Ligi ya
Tanzania walizozitumia kwenye mashindano ya Kombe la Kagame. Pia inapinga
Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kujiunga Simba kwa vile ana leseni ya kuchezea Azam
kwa msimu wa 2012/2013.
Pingamizi
lingine la Yanga kwa Simba ni kuwa imezidisha idadi ya wachezaji wa kigeni
wanaotakiwa kusajiliwa kwa maelezo inao wanane wakati wanaoruhusiwa ni watano.
Imewataja wachezaji hao kuwa ni Lino Masombo, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi, Mussa
Mude, Kanu Mbiyavanga, Pascal Ochieng, Komalmbil Keita na Daniel Akuffor.
Pingamizi
nyingine ambazo jumla zinahusu wachezaji 17 walioombewa usajili katika timu za
Ligi Kuu ni Toto Africans ya Mwanza imewawekea pingamizi wachezaji Enyinna
Darlington aliyeombewa usajili Kagera Sugar, na Mohamed Soud anayekwenda
Coastal Union kwa maelezo kuwa bado ina mikataba na wachezaji hao.
Pia
Flamingo ya Arusha inapinga usajili wa wachezaji wake Kelvin Friday Iddy katika
timu za Azam na Salim Walii (Polisi Mara) kwa vile taratibu za kuwahamisha bado
hazijafanywa. Nayo Kagera Sugar inapinga usajili wa beki David Charles Luhende
kwenda Yanga kwa vile ada ya uhamisho haijalipwa.
Super
Falcon ya Chanjamjawiri, Chakechake, Pemba inapinga wachezaji wake wanne;
Edward Christopher Shija, Samir Said Luhava (Simba), Robert Joseph Mkhotya
(African Lyon) na Sultan Juma Shija (Coastal Union) kusajiliwa katika timu hizo
kwa maelezo taratibu halali za uhamisho hazikufuatwa.
Mchezaji
Othman Hassan aliyeombewa usajili Coastal Union anapingwa na Oljoro JKT kwa
vile bado ana mkataba na timu hiyo unaomalizika Mei 24, 2013. Nayo Rollingstone
Multipurpose Ateclass Foundation ya Arusha inapinga usajili wa Kigi Makassy
kutoka Yanga kwenda Simba hadi itakapolipwa fidia ya kumlea mchezaji huyo kwa
vile bado hajafikisha umri wa miaka 23.
0 comments:
Post a Comment