Na Ally Mohamed,
Zanziabr
MABINGWA watetezi
wa Ligi Kuu Zanzibar, Super Falcon wameendelea kuboronga katika ligi hiyo licha
ya kumtimua kocha wake wiki iliyopita, baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Jamhuri
ya Pemba, kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba, wakati Bandari imeibuka na ushindi
wa 2-1 dhidi ya KMKM Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Uwanja wa
Gombani, Falcon ambao wataiwakilisha Zanzibar katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani,
walikubali kipigo cha tatu mfululizo katika ligi hiyo kwa mabao ya Mfaume
Shaaban na Abdallah Mohammed, hiyo ikiwa mechi ya nane kwa Super Falcon
kupoteza.
Bandari iliyopanda
Ligi Kuu msimu huu ilipata bao lake la kwanza dakika ya 37, lililotiwa kimiani
na Mussa Omar, kabla ya KMKM kusawazisha dakika ya 44, mfungaji Mudrik Muhib na
Bandari wakapata bao la ushindi dakika 76 kupitia kwa Mohammed Abdallah.
Ligi hiyo
inatarajia kuendelea tena kesho kwa mechi mbili, kisiwani Pemba, Chipukizi wakicheza
na Duma Uwanja wa Gombani, huku kisiwani Unguja, Malindi wakicheza na Mafunzo
katika uwanja wa Amaan.
0 comments:
Post a Comment