Coastal Union |
Na Prince Akbar
COASTAL
Union imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Kagera Sugar ya Bukoba, kwenye Uwanja
wa Mkwakwani mjini Tanga, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Ushindi huo, ulitokana na mabao ya Daniel Lyanga na Nsa Job mawili,
ni wa pili katika mechi nne za Wagosi wa Kaya tangu kuanza kwa Ligi Kuu, unakuja
siku moja baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Juma
Mgunda.
Mgunda,
alijiuzulu jana akisema ameamua kufanya hivyo mapema, kabla ya mambo
hayajaribika, ili mwalimu mpya anayekuja afanye kazi vizuri.
Akizungumza
na BIN ZUBEIRY jana, Mgunda alisema
kwamba anaachia timu baada ya kucheza mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, akiwa ameshinda moja na kutoa sare mbili.
“Kama
utaweza kuona naiacha timu ikiwa kwenye hali nzuri kuliko Yanga, ambao
wamefungwa mechi moja, sare moja na kushinda moja, naondoka kwa moyo mkunjufu,
sina kinyongo na mtu,”alisema.
Mgunda
alisema hiyo ndio hulka yake tangu anacheza Coastal Union, kuwa na moyo swafi
na ataendelea kuwa hivyo. “Mimi ni mpenzi wa Coastal Union, hakuna asiyejua, na
kwa manufaa ya timu, naondoka,”alisema.
Kumekuwa
kama kuna kampeni ya kumvuruga Mgunda kazini ambayo imekuwa ikiendeshwa kwenye
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kwa kumzomea kila timu inapocheza, hatimaye ameamua
kuwaachia timu.
Kwa sasa
Coastal, imebaki na kocha Msaidizi, Habib Kondo ambaye msimu uliopita alikuwa
kocha wa Villa Squad ya Kinondoni, iliyoshuka daraja na leo ndio kaiongoza timu
hiyo ya Barabara ya 13, katika mechi na Kagera Sugar.
Mgunda
anakuwa kocha wa pili wa Ligi Kuu kuachia timu, baada ya Mbelgiiji, Tom
Sainftiet ambaye amefukuzwa Yanga, baada ya kutofautiana na uongozi, akiwa
ameiongoza timu kwenye mechi mbili tu za Ligi Kuu, akitoa sare moja na kufungwa
moja. Hemed Morocco, kocha wa Mafunzo ya Zanzibar yupo kwenye mazungumzo na
uongozi wa Coastal Union ya Tanga, ili awe kocha mpya wa timu hiyo kufuatia
kubwagwa manyanga kwa Mgunda.
Katika mechi
nyingine ya ligi hiyo, Polisi Morogoro imelazimishwa sare na Toto African ya
Mwanza kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro jioni hii.
P W D L GF GA GD P
MSIMAMO WA LIGI KUU
BARA
Simba SC 3 3 - - 7 1 6 9
Azam FC 3 2 1 - 3 1 2 7
Coastal 3 2 1 - 5 3 2 7
JKT Oljoro 3 1 2 1 2 1 1 5
Mtibwa Sugar 3 1 1 1 3 1 2 4
Yanga SC 3 1 1 1 4 4 - 4
Toto African 3 - 3 1 3 2 1 3
Ruvu Shooting 3 1 - 2 4 5 -1 3
African Lyon 3 1 - 2 2 5 -3 3
JKT Ruvu 3 1 - 2 3 7 -4 3
Prisons 2 - 2 - 1 1 - 2
Polisi Moro 3 - 2 1 - 1 -1 2
Kagera Sugar 3 - 1 2 2 4 -2 1
JKT Mgambo 3 - - 3 1 3 -2 0
0 comments:
Post a Comment