// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CHUJI AANZA KAZI LEO YANGA, MTAKATIFU TOM ALIA SIMBA INABEBWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CHUJI AANZA KAZI LEO YANGA, MTAKATIFU TOM ALIA SIMBA INABEBWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, September 03, 2012

    CHUJI AANZA KAZI LEO YANGA, MTAKATIFU TOM ALIA SIMBA INABEBWA


    Mtakatifu Tom
    Na Mahmoud Zubeiry  
    KOCHA wa Yanga, Tom Saintfiet raia wa Ubelgiji amesema kwamba anatarajia viungo wake Athumani Iddi ‘Chuji’, Rashid Gumbo, Nizar Khalfan na Juma Seif ‘Kijiko’ wataanza mazoezi leo, lakini amelalamikia mno ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambayo inaonyesha wapinzani wao wa jadi, Simba SC watacheza mechi za mwanzo nyumbani.
    “Hii ni kupendelea Simba, dhahiri kucheza mechi sita za mwanzo Uwanja wa Taifa ni kipaumbele kwao,”alilalamika Santifiet alipozungumza na BIN ZUBEIRY asubuhi ya leo.
    Viungo hao walikosekana uwanjani juzi, wakati Yanga inashinda 2-1, kwa mabao ya mawili ya dakika za lala salama, dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
    Saidi Bahanuzi ‘Spider Man’, kwa mara nyingine jana alikuwa shujaa wa Yanga baada ya kufunga bao la ushindi dakika ya 85 katika mchezo, ambao Coastal Union ilimpoteza kiungo wake Jerry Santo aliyepewa kadi nyekundu kwa kumtolea maneno machafu refa Hashim Abdallah dakika ya 59.
    Hilo lilikua bao lake la nane Bahanuzi tangu aanze kuichezea Yanga miezi miwili iliyopita, akitokea Mtibwa Sugar. Awali ya hapo, beki Mganda, Philip Kaira alijifunga katika harakati za kuokoa krosi ya Shamte Ally dakika ya 84.    
    Hadi mapumziko, Coastal tayari walikuwa mbele kwa bao hilo moja lililotiwa kimiani na kiungo Razack Khalfan, aliyefumua shuti la umbali wa mita 26.
    Razack alitokea Yanga B mwaka 2008 na kupandishwa kikosi cha kwanza mwaka 2009, chini ya kocha Mserbia, Profesa Dusan Savo Kondic, lakini misimu miwili baadaye akatolewa kwa mkopo African Lyon, ambao umeisha na msimu huu amesaini Coastal.
    Kwa ujumla Razack, mdogo wa kiungo wa Yanga, Nizar Khalfan alicheza soka ya kusababisha swali kwa nini Yanga ilimuacha. 
    Mechi hiyo ilichezeshwa na refa Hashim Abdallah aliyechezesha pia mechi ambayo Yanga ililala 5-0 kwa Simba katika Ligi Kuu msimu uliopita, ambaye leo amesaidiwa na Shaffi Mohamed na Iddi Maganga.
    Awali, mchezo huo nusura uvunjike, baada ya kocha wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet kutoa timu uwanjani kutokana na kucheleweshwa kwa muda wa kuanza, ambao kimakubaliano ulikuwa saa 10:00 jioni.
    Lakini Coastal walichelewa kufika uwanjani (walifika saa 10:05 jioni ) na kuanza kwanza kupasha misuli moto, jambo ambalo lilimkera Saintfiet na kusistiza waachane na mazoezi yao mechi ianze, lakini makocha wa timu hiyo ya Tanga, Juma Mgunda na Habib Kondo waliendelea na biashara yao.
    Saintfiet akatoa timu yake uwanjani, kabla ya kwenda kubembelezwa na viongozi wake, ndipo akarejesha timu na mpira ukaanza saa 10:31 jioni.
    Kwa ujumloa Coastal walitawala kipindi cha kwanza mchezo huo na kipindi cha pili japokuwa mchezo ulikuwa wa pande zote mbili hata baada ya Santo kutolewa kwa kadi nyekundu, lakini Yanga waliuteka kabisa dakika 15 za mwishoni.
    Kwa Coastal, hiyo inakuwa mechi ya nne Coastal wanafungwa ndani ya mechi tano za kujipima nguvu, nyingine zikiwa dhidi ya Bandari mara mbili, 3-2 Mombasa na 2-0 Tanga na 2-1 dhidi ya Polisi mjini Morogoro, wakati mechi waliyoshinda ni dhidi ya JKT Oljoro 2-0.
    Kwa Yanga, chini ya kocha wake Mbelgiji, Saintfiet, hiyo inakuwa mechi ya 10 anashinda kati ya 11 alizocheza tangu ajiunge na kabu hiyo miezi miwili iliyopita.
    Kwa upande wake, kocha Saintfiet ameendeleza rekodi yake nzuri akishinda mechi ya 10 kati ya 11 alizoiongoza timu hiyo tangu ajiunge nayo miezi miwili iliyopita.

    REKODI YA SAINTFIET YANGA
    1.                      Yanga Vs JKT Ruvu 2-0
    2.                      Yanga Vs Atletico (Burundi) 0-2
    3.                      Yanga Vs Waw Salam (Sudan Kusini) 7-1
    4.                      Yanga Vs APR (Rwanda) 2-0
    5.                      Yanga Vs Mafunzo (Z’bar) 1-1 (5-3penalti)
    6.                      Yanga Vs APR (Rwanda) 1-0
    7.                      Yanga Vs Azam 2-0
    8.                      Yanga Vs African Lyon 4-0
    9.                      Yanga Vs Rayon (Rwanda) 2-0
    10.                    Yanga Vs Polisi (Rwanda) 2-1
    11.                    Yanga Vs Coastal Union 2-1
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHUJI AANZA KAZI LEO YANGA, MTAKATIFU TOM ALIA SIMBA INABEBWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top