|
Cheka anatisha |
Na Mahmoud Zubeiry
FRANCIS
Cheka ‘SMG’ wa Morogoro, ameendeleza ubabe dhidi ya mabondia wa Dar es Salaam,
baada ya kumtandika kwa Technical Knockout (TKO), raundi ya sita Karama
Nyilawila na kutwaa ubingwa wa UBO uzito wa Middle, kwenye ukumbi wa PTA,
Sabasaba, Dar es Salaam muda mchache uliopita katika pambano ambalo lilipangwa kuwa la raundi 12.
Karama aliingia
kwa kasi katika pambano hilo na kutumia nguvu nyingi kumshambulia Cheka, ambaye
alikuwa mtulivu akipangua na kukwepa ngumi nyingi za mpinzani wake huyo.
Kuna wakati
kwa kasi ya Karama na namna Cheka alivyokuwa akirudi nyuma kwa makonde ya
kusukumwa na mpinzani wake, wengi waliamini labda siku ya kuzima ubabe wa
bondia wa Morogoro imewadia.
Hata hivyo, raundi
tatu tu zilitosha kumaliza cheche za Karama na tofauti na randi za awali
alivyokuwa akirudi kwenye kona yake alikuwa akisimama, lakini baada ya raundi
hiyo, aliomba kiti, wakati mpinzani wake aliendelea kusimama.
Kuanzia raundi
ya nne, ilionekana dhahiri Karama ameishiwa nguvu na pumzi na ndipo Cheka
alipoanza kumshughulikia.
Katika raundi
ya sita, Cheka aliingia kwa kasi na akafanikiwa kumtandika mpinzani wake upper-cut
na hook iliyomkalisha chini. Alihesabiwa
hadi saba, akajikokota kuinuka, lakini mishipa ya kichwa ilikuwa bado haiwasiliani
hivyo akaamua kunyoosha mikono yake miwili juu, maana yake; amesalimu amri.
Hapo ndipo shangwe
zilipoibuka katika ukumbi wa PTA, watu wakimpongeza Cheka kuendeleza ubabe
wake.
|
Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
|
Refarii wa mpambano akiwaelekeza mabondia wasicheze kwa kukumbatiana |
|
Bondia Fransic Cheka kushoto akipepesuka baada ya kupigwa ngumi na Karama Nyilawila wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi cheka alishinda kwa K.O raundi ya sita na kufanikiwa kunyakuwa ubingwa picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com |
|
Bondia Fransic Cheka kushoto akimshambulia Karama Nyilawila kwa masumbwi wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi Cheka alishinda raundi ya sita baada ya kumpiga na kudondoka chini baada ya kuesabiwa akashindwa kuendelea picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
|
Bondia Karama Nyilawila kulia akijitaidi kukwepa makonde ya mpinzani wake Fransic Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi cheka alishinda kwa K,o raundi ya sita picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
|
Mabondia Karama Nyilawila kushoto akionesheana umwamba wa kutupa masumbwi na Fransic Cheka wakati wa mpambano wao cheka alishinda kwa K,O Raundi ya sitapicha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
|
Fransic Cheka kushoto na Karama Nyilawila wakiwa uringoni kuoneshana uwezo wa kutupiana masumbwi Cheka alishjnda kwa K,O ya Raundi ya sita picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
|
Mabondia Karama Nyilawila kushoto na Fransic Cheka wakionesheana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Cheka alishinda kwa K,o raundi ya sitapicha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
|
Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
|
Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
|
Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
0 comments:
Post a Comment