|
Kikosi cha Coastal kilichoanza |
|
Kikosi cha Azam kilichoanza |
|
Makocha Juma Mgunda kulia akiwa na Msaidizi wake, Habib Kondo |
|
Kipute |
|
Kipute |
|
Pasi imefika |
|
Pasi inasafiri |
|
Nahodha Aggrey Morris kulia akitafuta mbinu za kumtoka kipa wa Coastal, Jackson Chove kushoto |
|
Bocco 'Adebayor' anasafiri |
|
Boris Bunjak, kocha wa Azam akiwapa maelekezo wachezaji wake wakati mchezo ukiendelea |
|
John Bocco anakosa la wazi |
|
Bocco anafunga la pili |
|
Bocco anafunga la kwanza |
Na
Princess Asia
MABAO mawili ya John Raphael Bocco ‘Adebayor’ katika
dakika za 15 na 44, leo yameipa Azam FC ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal
Union ya Tanga katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii
dhidi ya Simba SC, Septemba 11, mwaka huu, Uwanja wa Chamazi.
Bocco alikuwa mwiba mchungu kweli leo kwa safu ya
ulinzi ya Coastal, kwani pamoja kufunga mawili, lakini alikosa mabao matatu ya
wazi mno. Abdulhalim Humud alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 32 kwa
rafu na lugha chafu.
Hiyo ni mechi ya tano Coastal inafungwa kati ya sita
za kujipima nguvu ilizocheza kabla ya jana kufungwa 2-1 na Yanga, awali ilifungwa
3-2 na Bandari mjini Mombassa, baadaye 2-0 Tanga, ilifungwa 2-1 na Polisi mjini
Morogoro na yenyewe iliifunga JKT Oljoro 1-0.
Kwa Azam hii ni mechi ya tatu mfululizo wanashinda, awali
waliifunga 1-0 Prisons ya Mbeya na Transit Camp 8-0.
Azam inatarajiwa kuivaa Simba katika mechi ya Ngao
ya Jamii ya kuashiria kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara, Septemba 11, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ikiwa ni mchezo
wake wa kwanza katika historia ya Ngao hiyo.
Kihistoria hiyo itakuwa mechi ya tano ya Ngao ya
Jamii kuchezwa nchini na ya pili kuishirikisha timu nje ya wapinzani wa jadi wa
soka ya Tanzania, Simba na Yanga.
Mtibwa ilicheza na Yanga mwaka 2009, baada ya Simba
kugoma na ikashinda mabao 2-1 na kutwaa Ngao, wakati kabla ya hapo, mwaka 2001,
Ligi Kuu ya Tanzania ikiwa bado inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
kupitia bia ya Safari Lager, ilichezwa mechi ya kwanza ya Ngao kihistoria.
Katika mechi hiyo, Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi
ya Simba na mwaka juzi Yanga iliifunga tena Simba kwa penali 3-1 kufuatia sare
ya 0-0 na mwaka jana, Simba ilitwaa Ngao ya kwanza katika historia yake, kwa
kuifunga Yanga mabao 2-0.
Ikumbukwe mara ya mwisho Simba SC ilipokutana na
Azam FC, katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la
Kagame mwezi uliopita Dar es Salaam, ilifungwa mabao 3-1, yote yakifungwa na
Bocco na lile la kufutia machozi kwa wekundu hao Msimbazi liliwekwa kimiani na
beki mahiri Shomari Kapombe, aliyemajeruhi kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment