Boban anavyoshughulikaga |
Na Mahmoud Zubeiry
HARUNA Moshi
Shaaban, ni mchezaji pekee ambaye hayupo kambini Simba SC, lakini anaweza
kwenda leo au kesho kuungana na wenzake, visiwani Zanzibar kwa maandalizi ya
mchezo dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Yangas SC.
Japo Boban
hayupo kambini Zanzibar, lakini Simba SC inaendelea vizuri na maandalizi yake
ya pambano dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC, Oktoba 3, mwaka huu, ikifanya
mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Kiislam, Kwerekwe, visiwani Zanzibar na kambi
yao ipo Chukwani.
Morali ya
kambi ipo juu na wachezaji wote wako fiti, wakijifua kwa shauku kubwa ili
kumvutia kocha Mserbia, Milovan Cirkovick awape nafasi ya kucheza Oktoba 3,
kuanzia sa 1:00 usiku.
Simba
itarejea Dar es Salaam Jumamosi kucheza mechi na Prisons ya Mbeya Uwanja wa
Taifa, kisha kurejea tena visiwani humo kuendelea na maandalizi ya mchezo wa
Jumamosi ijayo.
Hata hivyo,
katika michezo miwili ijayo, Simba itamkosa mshambuliaji wake Mganda, Emmanuel
Okwi ambaye amefungiwa na Kamati ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, chini ya
Mwenyekiti wake, Wallace Karia kufuatia kikao cha juzi, sambamba kumtoza faini
ya Sh. 500,000 kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa JKT Ruvu, Kessy Mapande.
Okwi
alifanya hivyo akilipa kisasi cha kuchezewa rafu Jumatano iliyopita, Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Tayari Okwi
amekosa mechi moja ya juzi dhidi ya Ruvu Shooting na wakati, na sasa atakosa mechi
mbili zaidi, dhidi ya Prisons na dhidi ya Yanga na baada ya hapo atakuwa huru
kuendelea kumtukia mwajiri wake.
Siyo siri,
kuelekea pambano la watani wa jadi, Okwi alikuwa ni homa kwa Yanga, hasa
wakikumbuka namna alivyowanyanyasa katika mechi iliyopita, akifunga mabao
mawili kwenye ushindi wa 5-0 na kusababisha mawili.
0 comments:
Post a Comment