Azam FC |
Na Prince Akbar
LIGI Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara, leo inaingia katika mzunguko wake wa nne kwa mechi za
Super Weekend, ambazo zitaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha
SuperSport cha Afrika Kusini.
Mechi ya
kwanza ambayo itachezwa leo itakuwa kati ya Azam FC na JKT Ruvu Stars, itakayofanyika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku kwa viingilio vya Sh.
3,000 mzunguko, sh. 5,000 kwa VIP C na VIP B wakati VIP A kiingilio kitakuwa
sh. 10,000.
Kesho kutakuwa
na mechi kati ya Simba na Tanzania Prisons itakayofanyika Uwanja wa Taifa, pia
mjini Dar es Salaam kuanzia saa 11:00 jioni, wakati Yanga na African Lyon
zitapambana keshokutwa kwenye Uwanja huo huo kuanzia saa 11:00 jioni.
Uwanja wa Chamazi,
maarufu kama Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam wenyewe utakuwa
mwenyeji wa mechi kati ya Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar itakayochezwa Oktoba 1,
mwaka huu kuanza saa 10:30 jioni.
Mechi ya
mwisho ya Super Weekend itachezwa Oktoba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam ikwakutanisha watani wa jadi, Yanga na Simba kuanzia saa 1:00 usiku.
Wakati huo
huo: Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo
cha Katibu Mkuu mstaafu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Erasto Zambi
kilichotokea juzi mjini Dar es Salaam kutokana na maradhi.
Zambi ambaye
anatarajiwa kuzikwa Jumapili, kabla ya kuwa kiongozi TOC, kwa muda mrefu
alikuwa mwalimu wa michezo katik Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambapo
wanamichezo wengi hasa waliokuwa wanafunzi katika chuo hicho wamepita kwake.
Msiba huo
ambao uko nyumbani kwake Ubungo Kibangu, Dar es Salaam ni pigo kwa familia ya
Zambi, TFF na wanamichezo kwa ujumla nchini kutokana na mchango na mawazo
aliyotoa kwa shirikisho wakati akiwa kiongozi wa TOC.
TFF imetoa
pole kwa familia ya Zambi, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na uvumilivu
katika kipindi hiki cha msiba huo mzito.
MSIMAMO WA LIGI KUU
BARA
P W D L GF GA GD P
Simba SC 3 3 - - 7 1 6 9
Azam FC 3 2 1 - 3 1 2 7
Coastal 3 2 1 - 5 3 2 7
JKT Oljoro 3 1 2 1 2 1 1 5
Mtibwa Sugar 3 1 1 1 3 1 2 4
Yanga SC 3 1 1 1 4 4 - 4
Toto African 3 - 3 1 3 2 1 3
Ruvu Shooting 3 1 - 2 4 5 -1 3
African Lyon 3 1 - 2 2 5 -3 3
JKT Ruvu 3 1 - 2 3 7 -4 3
Prisons 2 - 2 - 1 1 - 2
Polisi Moro 3 - 2 1 - 1 -1 2
Kagera Sugar 3 - 1 2 2 4 -2 1
JKT Mgambo 3 - - 3 1 3 -2 0
0 comments:
Post a Comment