Na Prince Akbar
AZAM FC
imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuifunga JKT
Ruvu mabao 3-0, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, katika mechi iliyoanza
saa 1:00.
Mabao ya
Azam katika mchezo huo, yalifungwa na John Raphael Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 44
kwa penalti, Kipre Herman Tcheche dakika ya 65 na Kipre Michael Balou dakika ya
79.
Ushindi huo,
moja kwa moja unaipandisha Azam kileleni mwa ligi hiyo, ikifikisha pointi 10
baada ya kucheza mechi nne na kuipiku Simba SC, yenye pointi tisa, lakini iko
nyuma kwa mchezo mmopja.
Kesho Simba itacheza
na Tanzania Prisons itakayofanyika Uwanja wa Taifa, pia mjini Dar es Salaam
kuanzia saa 11:00 jioni, wakati Yanga na African Lyon zitapambana keshokutwa kwenye
Uwanja huo huo kuanzia saa 11:00 jioni.
Uwanja wa Chamazi,
maarufu kama Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam wenyewe utakuwa
mwenyeji wa mechi kati ya Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar itakayochezwa Oktoba 1,
mwaka huu kuanza saa 10:30 jioni.
Mechi ya
mwisho ya Super Weekend itachezwa Oktoba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam ikwakutanisha watani wa jadi, Yanga na Simba kuanzia saa 1:00 usiku.
0 comments:
Post a Comment