Tetesi za Jumanne magazeti Ulaya
ARSENAL KUSAJILI BEKI KINDA NI BALAA, LINACHEZA KATI, KULIA NA KIUNGO PIA
Arsenal ilituma wasaka vipaji wake kumtazama mchezaji anayewaniwa na Manchester United, Liam Moore katika mechi ya Leicester mwishoni mwa wiki iliyopita. Kinda huyo wa umri wa miaka 19, ambaye anacheza vizuri beki ya kati, beki ya kulia au kiungo, amekuwa kivutio katika Ligi Daraja la Kwanza msimu huu.
Liverpool haina mpango wa kumsajili mshambuliaji wake wa zamani, Michael Owen licha ya ubutu wa safu yake ya ushambuliaji hivi sasa, na mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 32 anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili atakaolipwa pauni Milioni 1.5 kwa msimu na Stoke.
Mshambuliaji wa West Brom, Peter Odemwingie, mwenye umri wa miaka 31, amesema alifikiria kuondoka Hawthorns kipindi hiki.
West Ham inataka kumsajili beki wa zamani wa kati wa Sunderland, John Mensah, mwenye umri wa miaka 29, kama mchezaji huru, kufuatia klabu yake, Lyon ya Ufaransa kuamua kutomuongezea mkataba.
TORRES AAHIDI MAKUBWA CHELSEA
Fernando Torres, mwenye umri wa miaka 28, amewaahidi Chelsea "Msimu wa kutisha" hivi sasa akiwa mshambuliaji chaguo la kwanza, kufuatia kuondoka kwa Didier Drogba.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kwamba kiungo Jack Wilshere, mwenye umri wa miaka 20, atakuwa fiti kuanza katika mechi tena "ndani ya mwezi" baada ya kuwa majeruhi kwa zaidi ya mwaka.
HULK AAHIDI SOKA YA KIUNGWANA
Mshambuliaji mpya wa Zenit St Petersburg, Hulk, mwenye umri wa miaka 26, ameahidi kucheza soka ya kiungwana katika mechi yake ya mwisho akiwa na jezi ya Porto Jumamosi. Aligoma kuwarudishia mpira wapinzani katika kitendo cha fair play na kujaribu kutaka kufunga.
0 comments:
Post a Comment