Kelvin Yondan |
Na Princess Asia
KAMATI ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa inatarajia kukutana Jumapili (Septemba 2 mwaka huu) kupitia usajili wa wachezaji kwa msimu wa 2012/2013.
Usajili utakaopitiwa ni wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Lidi Daraja la Kwanza (FDL) ambapo Kamati itapitia pingamizi zilizowasilishwa na klabu mbalimbali dhidi ya wachezaji waliosajiliwa na klabu zingine.
Miongoni mwa masuala yanayotarajiwa kujadilika katika kikao hicho ni usajili wa beki Kevin Yondan kutoka Simba kwenda Yanga na usajili wa kiungo Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kutoka Azam FC kwenda Simba SC.
Ni kesi zinazofanana- kwa Redondo anadaiwa kusaini Simba wakati bado hajamaliza mkataba wake Azam FC sawa na Yondan, anadaiwa kusaini Yanga wakati bado ana mkataba na klabu yake, Simba SC.
Wachezaji wote wawili wamekanusha kuwa na mikataba na klabu zao za awali na Kamati ya Mgongolwa inatarajiwa kutoa jibu juu ya mustakabali wa wachezaji hao msimu ujao watacheza wapi.
0 comments:
Post a Comment