// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA WAPELEKA KOMBE BUNGENI, MAMA KARUME KUMUAPISHA MANJI KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA WAPELEKA KOMBE BUNGENI, MAMA KARUME KUMUAPISHA MANJI KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, August 04, 2012

    YANGA WAPELEKA KOMBE BUNGENI, MAMA KARUME KUMUAPISHA MANJI KESHO


    Yanga watapeleka Kombe Bungeni Jumatatu
    Na Prince Akbar
    MAMBO mawili zaidi makubwa Yanga, ukiacha suala la Said Bahanuzi na Didier Kavumbangu, kesho majira ya saa 4:00 asubuhi, uongozi mpya wa Yanga ‘utaapishwa’ na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu hiyo, Mama Fatuma Karume, makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
    Baada ya hapo, Wachezaji na viongozi wa Yanga watasafiri kwenda Dodoma, kwa ajili ya mwaliko wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wapenzi wa klabu hiyo, Jumatatu.
    Wabunge hao, wamewaalika wachezaji wa Yanga, baada ya kutwaa taji la Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Jumamosi iliyopita, wakiifunga Azam FC mabao 2-0 kwenye fainali, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Julai 15, mwaka huu, Yanga ilipata viongozi wapya, ambao ni Mwenyekiti Yussuf Manji, Makamu wake, Clement Sanga na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji, Abdallah Bin Kleb, George Manyama na Mussa Katabaro.
    Hao wanaungana na Wajumbe wengine waliosalia kutoka uongozi uliochaguliwa mwaka juzi, Mohamed Bhinda, Titto Osoro, Salim Rupia na Sarah Ramadhan, baada ya wajumbe wengine, wakiwemo Mwenyekiti, Wakili Lloyd Nchunga na Makamu wake, Davis Mosha kujiuzulu.    
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA WAPELEKA KOMBE BUNGENI, MAMA KARUME KUMUAPISHA MANJI KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top