Na Princess Asia
WAKATI
zimebaki wiki mbili kabla ya kuanza kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, hali ya viwanja vingi ni mbaya na hakuna jitihada ya kuviboresha
kabla ya kuanza kwa ligi hiyo.
Uchunguzi
uliofanywa na BIN ZUBEIRY, umegundua kwamba ni viwanja vinne tu kati ya
viwanja 10 vinavyotarajiwa kutumika kwa ajili ya ligi hiyo ndio vipo katika
hali nzuri, inayokidhidi vigezo.
Viwanja
hivyo ni Taifa, Dar es Salaam, ambao utatumiwa na klabu za Yanga na Simba, Chamazi
wa Azam, ambao unaweza kutumiwa pia na African Lyon na JKT Ruvu, Manungu wa
Mtibwa Sugar na CCM Kirumba wa Toto African.
Viwanja
vingine, Mabatini uliopo Chalinze wa Ruvu Shooting, Mkwakwani, Tanga wa Coastal
Union na Mgambo Shooting, Jamhuri Morogoro wa Polisi, Kaitaba, Bukoba wa Kagera
Sugar, Sheikh Amri Abeid, Arusha wa JKT Oljoro na Sokoine, Mbeya wa Prisons vipo
katika hali mbaya.
Viwanja
vingi kati ya hivyo, eneo lake la kuchezea ni gumu, kuna mabonde na hata nyasi
zake hazijastawi vizuri, hali ambayo inahatarisha hata maisha ya wachezaji wenyewe
kuumia. Hakuna dalili za jitihada haswa aidha za uongozi wa serikali za mikoa
au vyama vya soka vya mikoa husika kuboresha viwanja hivyo kabla ya kuanza kwa
Ligi Kuu.
Ligi
Kuu itaanza Septemba 15 mwaka huu, kwa timu zote 14 kujitupa kwenye viwanja
tofauti na mechi za ufunguzi zitakuwa kati ya Simba vs African Lyon (Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam), Polisi Morogoro vs Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro),
Tanzania Prisons vs Yanga (Sokoine, Mbeya), Mgambo JKT vs Coastal Union
(Mkwakwani, Tanga), JKT Ruvu vs Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam),
Kagera Sugar vs Azam (Kaitaba, Bukoba) na Toto Africans vs Oljoro JKT (Kirumba,
Mwanza).
Mzunguko
wa kwanza (first round) utamalizika Novemba 11 mwaka huu ambapo kwenye mzunguko
huo mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba itachezwa Oktoba 3 mwaka huu kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ligi
hiyo itamalizika Mei 18 mwakani kwa mechi kati ya Toto Africans vs Ruvu
Shooting (Kirumba), Mgambo JKT vs African Lyon (Mkwakwani), JKT Ruvu vs Mtibwa
Sugar (Azam Complex), Tanzania Prisons vs Kagera Sugar (Sokoine), Simba vs
Yanga (Uwanja wa Taifa), Oljoro JKT vs Azam (Sheikh Amri Abeid Kaluta) na
Polisi Morogoro vs Coastal Union (Jamhuri).
Endapo
Simba na Azam hazitafanikiwa kuvuka hatua mojawapo ya michuano ya Ligi ya
Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, ratiba hiyo itafanyiwa marekebisho.
Wakati
huo huo: Mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria ufunguzi rasmi wa
Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2012/2013 kati ya bingwa mtetezi Simba na
makamu bingwa Azam itachezwa Septemba 11 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
0 comments:
Post a Comment