Tetesi za Alhamisi magazeti ya Ulaya
VAN PERSIE AMWAGA WINO JUVE
NAHODHA wa Arsenal, Robin van Persie tayari amesaini mkataba na Juventus, kwa mujibu wa wakala wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Fabio Parisi.
Chelsea imekwama kumpata kwa dau la pauni Milioni 5.4, beki wa kulia wa Marseille, Cesar Azpilicueta, mwenye umri wa miaka 22, lakini inatarajiwa kuboresha ofa yake.
Barcelona imeungana na Chelsea na Real Madrid katika mbio za kuwania saini ya nyota wa Brazil, Neymar, mwenye umri wa miaka 19.
Tottenham Hotspur inamuwania kipa wa kimataifa wa Uholanzi, Maarten Stekelenburg, mwenye umri wa miaka 29, anayedakia AS Roma ya Italia.
WINGA wa kimataifa wa Slovakia na Manchester City, Vladimir Weiss, mwenye umri wa miaka 22, anajiandaa kwenda kucheza kwa mkopo Pescara ya Italia katika Serie A.
Lazio inataka kumsajili beki wa Newcastle, Davide Santon mwenye umri wa miaka 21 .
Wolves imesema kwamba itamuuza mshambuliaje wake mwenye umri wa miaka 25, Steven Fletcher, licha ya kukataa dau la pauni Milioni 10 kutoka Sunderland.
Fulham inataka kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kwa kuwasajili washambuliaji wa Huddersfield, Jordan Rhodes na Andrey Arshavin wa Arsenal.
Nyota wa Swansea, Joe Allen yupo karibu kukubali kusaini mkataba na Liverpool.
KOCHA wa Everton, David Moyes amekuwa mjini Copenhagen kumfuatilia beki wa kushoto wa Denmark, Bryan Oviedo, mwenye umri wa miaka 23.
ANDY CARROLL ATEMWA LIVERPOOL
Liverpool imesema kwamba Andy Carroll ametemwa kwenye kikosi cha mechi ya Europa League leo dhidi ya FC Gomel, kwa sababu ya majeruhi.
Mwenyekiti wa Chama cha Soka England (FA), David Bernstein ameahidi kuboresha mapambano dhidi ya ubaguzi katika soka.
WEST BROM KUWATUZA WEUSI WAKE WA 1970
West Brom imeungwa mkono katika mpango wake wa kuwatunukia tuzo za heshima wachezaji wake watatu weusi wa miaka ya 1970, Cyril Regis, Brendon Batson na marehemu Laurie Cunningham.
0 comments:
Post a Comment