Richard Mongustino |
Na Princess Asia
KIONGOZI wa zamani wa
bendi ya Diamond Sound ‘Dar es Salaam Kibinda Nkoi’, Ibonga Katumbi ‘Jesus’
mwezi ujao ataungana na baadhi ya wanamuziki wengine wa kundi hilo katika
onyesho la Usiku wa Sauti na Marafiki wa Kweli litakalofanyika katika mikoa ya
Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Zanzibar.
Akizungumza mjini Dar
es Salaam jana, mratibu wa tamasha hilo Martin Kadinda ‘Single Button’ alisema
onyesho hilo linahusisha wanamuziki wakongwe ambao wataungana na Jesus pamoja
hao wa Diamond.
“Kila kitu kinaenda sawa
aliyekuwa amealikwa kwenye onyesho ni Jesus lakini katika onyesho hilo
atatakiwa kuimba nyimbo zake kadhaa ambazo alitamba nazo akiwa Diamond na Beta
Musica kwa hali hiyo alishauri aite wenzake ili wamsindikize.
“Kutokana na heshima
walijengeana wenzake walikubali kumsindikiza, kwa hiyo mashabiki wa Kibinda
Nkoi baada ya miaka 12 wataweza kuwaona tena Ibonga Katumbi, Richard
Mangustino, Wayne Zola Ndonga na Alain Mulumba Kashama wakisimama pamoja na
kuimba tena nyimbo zao kali,” alisema Kadinda.
Kadinda alisema lengo
kubwa la onyesho hilo ni kuthamini muziki wa zamani na kufundisha matumizi ya
vyombo vya muziki.
Katika onyesho hilo pia
watakuwepo wapiga magitaa kama Elly Chinyama, Adolph Mbinga, Marcis Mengi na
mpiga drum wa mwisho kuipigia Diamond Sound Kata Nyama Serikali.
Baadhi ya nyimbo
zitakazopigwa katika onyesho hilo ni pamoja na Neema, Mugheni, Chance, Jetou,
Bana Beta, Midabwada na Infarouge. Kadinda alisema wanamuzki wengine
watakaoshiriki kwenye onyesho hilo wataendelea kutangazwa.
0 comments:
Post a Comment