Tetesi za Jumapili magazeti ya Ulaya
MAN UNITED YATAKA KUSAJILI KIUNGO WA MOURINHO REAL MADRID
Manchester United ina matumaini ya kuwapiku Arsenal katika kuwania saini ya Nuri Sahin, mwenye umri wa miaka 23, kutoka Real Madrid kwa mkopo kwa kutangaza na ofa ya kumnunua moja kwa moja.
Santi Cazorla amekutana na wachezaji wenzake wa Arsenal, baada ya kiung huyo mwenye umri wa miaka 27 kukamilisha vipimo na uhamisho wa dau la pauni Milioni 20 kutoka Malaga.
Manchester United imekubali kutoa pauni Milioni 30 kwa ajili ya Mbrazil, Lucas Moura, mwenye umri wa miaka 19, na inapanga kuongeza juhudi katika kuwania saini ya Robin van Persie.
Brendan Rodgers anajiandaa kuingia kwenye mnada wa mikopo ili kuimarisha kikosi chake cha Liverpool.
MCHEZAJI mpya wa Aston Villa, Ron Vlaar amemshauri mchezaji mwenzake wa Uholanzi, Robin van Persie asiende Juventus, kwa kuwa ni mshambuliaji huyo wa Arsenal aliyemvutia yeye kuja kucheza England.
Manchester City inataka kumsajili winga wa Swansea City na kikosi cha Olimpiki cha Uingereza, Scott Sinclair mwenye umri wa miaka 23.
Arsenal inatumai kwamba Robin van Persie atabaki katika klabu hiyo, baada ya Mholanzi huyo kuvutiwa na jitihada za kuboresha kikosi cha Washika Bunduki hao.
NYOTA wa Manchester City, Nigel de Jong, mwenye umri wa miaka 27, anatakiwa na Arsenal na Inter Milan ambazo zote zinataka kuimarisha safu zao za kiungo.
Tottenham imekata tamaa na Emmanuel Adebayor na sasa inaelekeza nguvu zake katika kuwania saini ya mshambuliaji wa Kibrazil, Leandro Damiao, mwenye umri wa miaka 23.
Brendan Rodgers anataka kumsajili beki wa Swansea, Ashley Williams, mwenye umri wa miaka 28, atue Liverpool kama mbadala wa Daniel Agger, anayetakiwa na Manchester City.
Juventus sasa inataka kumsajili Salomon Rondon baada ya kuona haiwezi kumpata tena Robin van Persie.
0 comments:
Post a Comment