Twite baada ya kutua Uwanja wa ndege akiwa na viongozi wa Yanga |
Shabiki wa Yanga Babu Ally, akiwa na jezi ya Rage na4 |
Twite akizungumza na Waandishi huku amevaa jezi namba 4 yenye jina Rage |
Mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya Yanga, Francis Kifukwe kushoto akiwa Uwanja wa Ndege na kigogo wa Usajili, Seif Ahmad 'Magari' |
Na
Mahmoud Zubeiry
BEKI
mpya wa Yanga, Mbuyu Twite ametua Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere na
kulakiwa na mamia ya wapenzi wa klabu hiyo, kabla ya kupakiwa kwenye gari
kuelekea makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
Hakuna
kiongozi yeyote wa Simba wala askari polisi aliyemsogelea kama ambavyo kulikuwa
kuna tishio kwamba akitua tu beki huyo wa kimataifa wa Rwanda, mwenye asili ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) watamkamata kwa tuhuma za kuwatapeli
dola za Kimarekani 30,000.
Inadaiwa,
kabla ya kusaini Yanga, Twite aliyekuwa akichezea APR ya Rwanda alisaini Simba
na kuchukua dola 30,000.
Hata
hivyo, baadaye mchezaji huyo alighairi na kuamua kwenda Yanga na kurudisha
fedha za Simba kupitia viongozi wa APR na St Eloi Lupopo ya DRC, ambazo
zilikuwa zinammiliki kwa pamoja mchezaji huyo.
Lakini
viongozi wa Simba waligoma kupokea fedha hizo ingawa viongozi wa APR na Lupopo
walifika hadi ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutaka kuzikabidhi
fedha hizo, ili Simba wakazichukulie hapo.
Twite
aliianza kuichezea Yanga wiki iliyopita ilipokuwa Kigali, Rwanda kwa ziara ya
wiki moja lakini alishindwa kurejea na wenzake Jumatatu kwa kile kilichoelezwa
anakamilisha kuhama kwake rasmi na kuja kuanza maisha mapya Dar es Salaam,
Lakini
upande wa pili, Simba SC waliamini beki huyo amekwepa kukamatwa kufuatia kuvuja
kwa habari za mpango wa kumtegea akitua nchini wamkamate.
Ametua
na amekwenda Jangwani, maana yake jaribio la kumkamata akitua limefeli na sasa
tusubiri kama Simba watamuwekea mtego mwingine.
0 comments:
Post a Comment