Katibu wa CECAFA,
Nicholas Musonye akizungumza na mwasisi wa CECAFA, Kezekia Ssegwanga Musisi
kabla ya uzinduzi wa michuano ya mwaka huu ya Tusker katika hoteli ya Serena
mjini Kampala leo.
|
Katibu Mkuu wa CECAFA,
Nicholas Musonye akipokea Kombe la mwaka huu la Tusker kutoka kwa Mutahi katika
hoteli ya Serena mjini Kampala leo. Kulia ni rais wa FUFA, Livingstone
Kyambadde.
|
Mkurugenzi wa Masoko wa
Kampuni ya Bia Afrika Mashariki (EABL), Lemmy Mutahi (katikati) akikabidhi mfano wa hundi kwa
Katibu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas
Musonye. Kulia kabisa ni rais wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Livingstone
Kyambadde mjini Kampala leo.
|
Na Mahmoud Zubeiry
KAMPUNI ya Bia Afrika
Mashariki (EABL), kupitia bia yake ya Tusker Lager, leo imetangaza udhamini wa
dola za Kimarekani 450,000 kwa ajili ya michuano ya mwaka huu ya Kombe la CECAFA
–Tusker Challenge Cup itakayofanyika mjini Kampala, Uganda.
Baraza la Vyama vya
Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) pia imesema mashindano hayo yataanza Novemba
24 kwenye Uwanja wa Taifa wa Mandela, Namboole na kufikia tamati Desemba 8.
Katibu wa CECAFA,
Nicholas Musonye alitua Kampala Jumatatu kwa maandalizi ya michuano hiyo na leo
wamezindua rasmi kwenye hoteli ya Serena Hotel mjini Kampala na Meneja Masoko
wa EABL, Lemmy Mutahi amesema lengo la michuano hiyo ni kuzisaidia maandalizi
timu za Afrika Mashariki na Kati katika kuwania tiekti ya kucheza Fainali za
Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Musonye alisema
udhamini huo ni ongezeko la aslimia 5, kutoka michuano ya mwaka jana mjini Dar
es Salaam, ambayo Uganda waliibuka mabingwa.
Musonye alisema
udhamini huo utahusu usafiri, malazi na huduma nyingine, wakati jumla ya dola
za Kimarekani 60.000 zitakuwa kwa ajili ya zawadi, bingwa akipewa dola 30.000,
tmshindi wa pili dola 20.000 na dola 10.000 mshindi wa tatu. Musonye alisema mechi zote zitaonyeshwa na
Televisheni ya Super Sport.
0 comments:
Post a Comment