Mh Machano Othman Said akimkabidhi vifaa mwakilishi
wa Jamhuri ya Pemba, kulia ni Fimbo Bittala na Makamu wa Rais wa Chama cha Soka
Zanzibar (ZFA), Ally Mohamed.
|
Na
Prince Akbar
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imeipongeza
Grand Malt kwa kudhamini Ligi Kuu, ambapo kwa sasa inaamini itakuwa yenye
ushindani mkubwa.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa
timu 12 zinazoshiriki ligi hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Zanzibar Ocean View
leo, Waziri Asiye na Wizara Maalum katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ),
Machano Othman Said, alisema huo ni mwanzo mzuri kwa soka la Zanzibar.
“Huu ni mwanzo mzuri kwa soka la Zanzibar na naamini
tutafikia mafanikio yale tuliyokusudia. Nawashukuru Grand Malt kwa hili.
“Ila ninawaomba wadau wote wa ligi hii kuanzia Grand
Malt, ZFA (Chama cha Soka Zanzibar) na klabu viweke wazi mikataba yote ili
kusiwe na manung’uniko,” alisema.
Alizishauri klabu zote kufanya maandalizi mapema ili
kuweza kuifanya ligi hiyo iwe ya ushindani mkubwa na kuvitaka kuhakikisha zina
timu za vijana ili kuweza kupata timu bora kuanzia chini mpaka ngazi ya taifa.
Alisema ligi ilikosa msisimko katika miaka ya hivi
karibuni kutokana na lkukosa mdhamini na ana uhakika kwa sasa kila kitu
kitakuwa sawa.
Kwa upande wake, Meneja Masoka wa Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), watengenezaji wa Grand
Malt, Fimbo Butallah alisema wameamua kudhamini ili kuleta changamoto na
ushindani katika soka ya Zanzibar, kauli iliyoungwa mkono na Makamu wa Rais wa
ZFA, Ally Mohamed. Timu hizo zilikabibidhiwa jezi, mipira, vizuia ugoko pamoja na
vifaa vinginevyo.
Timu zinazoshiriki ligi hiyo ni pamoja na Super
Falcon, Jamhuri , Chipukizi, Duma, Mundu, Mafunzo, KMKM, Mtende, Malindi,
Bandari, Zimamoto na Chuoni.
0 comments:
Post a Comment