Felix Sunzu |
Na
Princess Asia
MSHAMBULIAJI
Mzambia wa Simba SC, ameondoka nchini leo nchini kuelekea Lubumbashi, Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuhudhuria msiba wa dada yake ambaye alifariki
dunia juzi jioni nchini humo.
Taarifa
ya Simba SC, imesema kwamba dada huyo wa mshambuliaji huyo, alikuwa amekwenda
kumtembelea ndugu yao, beki Stopila, anayechezea Tout Puissant Mazembe siku
sita zilizopita, lakini akakumbwa na umauti kutokana na ugonjwa wa Malaria ulimpanda
kichwani (Cerebral Malaria).
Uongozi
wa Simba umetoa pole kwa familia ya Sunzu pamoja na kufanikisha kuondoka kwa
haraka kwa mchezaji huyo ili akaungane na familia yake.
Sunzu
atarejea nchini baada ya kumaliza maziko na klabu ya Simba inaomba vyombo vya
habari na wadau wengine kumpa nafasi ya kuomboleza msiba huu mzito kwake
binafsi, kwa familia yake na Simba. Mola na aiweke roho ya marehemu mahali pema
peponi. Amen
0 comments:
Post a Comment