Said Bahanuzi 'Spider Man', mshambuliaji mpya Stars |
Na Prince Akbar
TIMU ya soka ya taifa
ya Tanzania, Taifa Stars Agosti 15 mwaka huu itapambana na Botswana ‘Zebras’
katika mchezo maalumu wa Kalenda ya FIFA utakaofanyika jijini Gaborone.
Tayari Kocha Kim
Poulsen alishatangaza kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini Agosti 8
mwaka huu tayari kwa mechi hiyo ya kirafiki ya kujipima nguvu.
Wachezaji wote
walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa
kuripoti kambi kwenye hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam, Agosti 8 mwaka huu saa
1 jioni tayari kwa mazoezi yatakayoanza siku inayofuata.
Makipa walioitwa kwenye
kikosi hicho ni Deogratias Munishi (Azam), nahodha Juma Kaseja (Simba) na
Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni nahodha msaidizi Aggrey Morris (Azam), Erasto
Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Athuman Idd
(Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Moshi (Simba), Mrisho Ngassa (Azam),
Mwinyi Kazimoto (Simba), Ramadhan Chombo (Azam), Ramadhan Singano (Simba),
Salum Abubakar (Azam) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John
Bocco (Azam), Mbwana Samatta (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-
DRC), Said Bahanuzi (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP
Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).
0 comments:
Post a Comment