. Asema hakuwa kumtaka Mrisho Ngassa Jangwani
. Ikitokea timu Tanzania kumpandia dau...
. Akoshwa na vitu vya dogo Simon Msuva, asema...
Na Mahmoud Zubeiry
BIN
ZUBEIRY inakuletea mahojiano ya maswali na
majibu na Kocha Mkuu wa mabingwa wa soka Afrika Mashariki na Kati, Yanga SC, Mbelgiji Tom Saintfiet 'Mtakatifu Tom' kuhusu masuala mbalimbali katika klabu yake. Endelea.
Mtakatifu Tom kushoto, akiwa na BIN ZUBEIRY |
BIN
ZUBEIRY: Habari za leo kocha?
SAINTFIET:
Nzuri, habari na wewe
BIN
ZUBEIRY: Salama. Vipi unaendeleaje na kazi?
SAINTFIET:
Vizuri
BIN
ZUBEIRY: Vipi kuhusu timu kwa ujumla?
SAINTFIET:
Timu yangu iko vizuri, isipokuwa wachezaji wachache ni wagonjwa. Haruna
Niyonzima, Nizar Khalfan, Rashid Gumbo, Juma Seif, Idrisa Assenga na Athumani
Iddi.
BIN
ZUBEIRY: Wanasumbuliwa na nini?
SAINTFIET:
Wengine Malaria, wengine mafua
BIN
ZUBEIRY: Sawa pole sana, hawajafanya mazoezi tangu lini?
SAINTFIET:
Wengine tangu Jumamosi, wengine walicheza Jumapili, lakini hakuna aliyefanya
mazoezi kabisa kati yao
BIN
ZUBEIRY: Sawa, nafikiri Simon Msuva ameleta changamoto mpya
kwako katika upangaji wa kikosi cha kwanza (safu ya ushambuliaji)
SAINTFIET:
Ndio, ananifurahisha sana
BIN
ZUBEIRY: sahihi, bado unajuta kumkosa Mrisho Ngassa?
SAINTFIET:
Sijawahi kujuta chochote, Ngassa ni mchezaji mzuri, lakini anachezea Simba,
hivyo hanihusu na siwezi kumzungumzia.
BIN
ZUBEIRY: Lakini alikuwa mbioni kujiunga na timu yako
SAINTFIET:
Sikuwahi kuhusishwa katika uhamisho wake, hakuna yeyote aliyenifuata kuomba
maoni yangu wala ushauri
Mtakatifu Tom na vijana wake |
BIN
ZUBEIRY: Ukiwa na Frank Domayo na Athumani Iddi ‘Chuji’
katika nafasi moja, upi mpango wako katika kikosi cha kwanza?
SAINTFIET:
Hilo siwezi kuongea kwenye vyombo vya habari sababu wote ni wachezaji wangu. Na
pia inategemea na mechi na mechi.
BIN
ZUBEIRY: Baada ya miezi miwili ya kuwa na Yanga, unaweza
kusema nini kuhusu klabu hiyo?
SAINTFIET:
Ninafurahia sana ushirikiano kutoka kwa wachezaji wangu na benchi la ufundi kwa
ujumla pamoja na viongozi
BIN
ZUBEIRY: Ikitokea klabu nyingine hapa nchini ikakupa ofa ya
mshahara mzuri zaidi unaopewa Yanga, utakubalia kuhamia huko?
SAINTFIET:
Haa haa, swali zuri sana, ina maana nihame Yanga nikipata ofa yoyote?
BIN
ZUBEIRY: Ndio, kutoka klabu yoyote nchini
SAINTFIET:
Sijawahi kusikia klabu yeyote inanitaka
BIN
ZUBEIRY: Ikitokea…
SAINTFIET:
Siwezi kuzungumzia mambo ambayo hayajatokea, kwa sababu inategemea na hali
halisi itakavyokuwa katika klabu yangu ya sasa wakati itakapotokea hiyo ofa
BIN
ZUBEIRY: Nini mipango yako ya muda mrefu katika timu?
SAINTFIET:
Nipo hapa kwa ajili ya kushinda ubingwa. Nachukia kufungwa. Nimecheza mechi 12
tangu nifike hapa, nimeshinda 11. Tangu mwaka 2008, nimefungwa mechi sita tu,
hivyo nataka kushinda popote ninapofanya kazi yangu ya ukocha
BIN
ZUBEIRY: Unahusika kwa namna yoyote katika timu ya vijana ya
Yanga?
SAINTFIET:
Ndio, kwa nini unauliza?
U20 ya Yanga mazoezini Kaunda |
BIN
ZUBEIRY: Nataka kujua
SAINTFIET:
Nataka kuhusika kikamilifu, kutokana na ukweli kwamba bado sijapewa gari, siwezi
kutekeleza hilo jukumu ipasavyo kwa sasa.
BIN
ZUBEIRY: Makocha wengi hata hapa Tanzania, mwishoni mwa msimu
hupandisha wachezaji kutoka timu zao za vijana, vipi wewe?
SAINTFIET:
Tunao Simon Msuva, Omega Seme, Frank Damayo, wote ni wachezaji wa timu ya
vijana…
BIN
ZUBEIRY: Lakini wote wametoka timu nyingine na kusajiliwa
Yanga, tena kwa fedha nyingi.
SAINTFIET:
Mradi wa maendeleo ya vijana siyo U20 , maendeleo ya vijana ni kuanzia U8, U10,
U12, U14, U16 na U18!
BIN
ZUBEIRY: Tutarajie
hilo siku moja katika Yanga chini ya utawala wako?
SAINTFIET:
Ningepeda pia, hilo lilikuwa moja ya maombi yangu kwa viongozi, nataka kujenga
akademi kama ya ASEC Mimosas. Nilikuwa Mkurugenzi wa Ufundi Nigeria na klabu ya
kulipwa Uholanzi. Nimewahi kuandika miradi ya maendeleo na ninajua vema namna
ya kuendesha akademi.
Ubingwa wa Kagame, matunda ya Mtakatifu Tom Jangwani |
BIN
ZUBEIRY: Tatizo nini kwa sasa katika klabu yako, Yanga?
SAINTFIET:
Oh, tunatakia kuanzia kwenye sifuri, tunahitaji malazi (kwa wachezaji), kocha
na huduma nyingine za muhimu kwa vijana.
BIN
ZUBEIRY: Huo ni mpango wako haswa katika Yanga?
SAINTFIET:
Ndio, kama klabu ikinipa sapoti katika hili. Nafikiri ni muhimu sana kwa Yanga
na soka ya Tanzania kwa ujumla, tunahitaji kuwa na akademi nzuri haswa.
Yanga katika Kombe la Kagame; Hapa ilikuwa ni Robo Fainali na Mafunzo wakati wa mikwaju ya penalti |
0 comments:
Post a Comment