Hans Poppe kushoto akimkabidhi jezi Ochieng kulia. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange 'Kaburu' |
Na Mahmoud Zubeiry
MABINGWA wa soka
Tanzania, Simba SC imesema inahisi dalili za kutotendewa haki katika usajili wake
kutoka ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Kwa nini? Mwenyekiti wa
Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba klabu yake
imekwishakamilisha usajili wa beki Paschal Ochieng kutoka AFC Leopard ya Kenya,
lakini ajabu TFF inashindwa kukamilisha uhamisho wa mchezaji huyo kwa mujibu wa
taratibu.
“Baada ya sisi
kumalizana na klabu na mchezaji, TFF wanatakiwa kutuma maombi ya ITC (Hati ya
Uhamisho wa Kimataifa) katika mfumo wa mtandao, kila tukiwapigia simu viongozi
wa FKF (Shirikisho la Soka Kenya) wanasema wanasubiri maombi kutoka TFF na bado
hayajatumwa, kwa kweli hii inasikitisha sana na tunahisi kuna dalili za kutotendewa
haki,”alisema Hans Poppe. BIN ZUBEIRY ilijaribu kuwasiliana nja Ofisa anayehusika na
masuala ya uhamisho wa kimataifa TFF, Sadi Kawemba, lakini kwa bahati mbaya
hakuwa karibu na simu yake, licha ya kupigiwa zaidi ya mara tatu. Awali, kulikuwa kuna
malalamiko kutoka AFC Leopard juu ya usajili wa Ochieng, lakini Simba
ikafanikiwa kumaliza utata huo kwa kuilipa klabu yake. Ochieng ni miongoni mwa
wachezaji watano wa kigeni watakaokuwamo kwenye kikosi cha Simba cha msimu
ujao, wengine wakiwa ni kiungo Komabil Keita, washambuliaji Felix Sunzu kutoka
Zambia, Emmanuel Okwi kutoka Uganda na Daniel Akuffo kutoka Ghana.
0 comments:
Post a Comment