Na Peince Akbar
MECHI ya kwanza ya
raundi ya kwanza kuwania tiketi ya kucheza Fainali za 10 za Afrika kwa vijana
chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwakani nchini Morocco kati ya Tanzania
(Serengeti Boys) na Kenya itachezwa Septemba 9 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex
ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN
ZUBEIRY mchana huu kwamba, tayari Serengeti Boys chini ya Kocha Mdenmark,
Jakob Michelsen na Msaidizi wake Jamhuri Kihwelo ikiwa na wachezaji 28 iko
kambini jijini Dar es Salaam tangu jana (Agosti 27 mwaka huu) kujiandaa kwa
mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni.
Amesema wachezaji
waliko kambini ni makipa Abdallah Bakar (Mjini Magharibi), Hamad Juma (Azam) na
Peter Manyika (JKT Ruvu). Mabeki ni Abdallah Salum (Mjini Magharibi), Basil
Seif (Morogoro), Hassan Mganga (Morogoro), Ismail Gambo (Azam), Mgaya Abdul
(Azam), Miraji Selemani (Polisi Morogoro), Miza Abdallah (Kinondoni), Mohamed
Hussein (Azam), Pascal Matagi (Dodoma) na Paul James (Kinondoni).
Viungo ni Farid Musa
(Kilimanjaro), Hussein Twaha (Coastal Union), James Mganda (Kipingu Academy),
Mbwana Ilyasa (Simba), Mohamed Haroub (Zanzibar), Mohamed Kapeta (Kinondoni),
Mudathiri Yahya (Azam), Mzamiru Said (Morogoro) na Selemani Bofu (JKT Ruvu).
Washambuliaji ni
Abdallah Kisimba (Mwanza), Calvin Manyika (Rukwa), Dickson Ambunda (Mwanza),
Joseph Lubasha (Azam), Kelvin Friday (Azam) na Salvatory Nkulula (Kipindu
Academy).
Mechi ya marudiano
itachezwa jijini Nairobi, Kenya kati ya Septemba 21, 22 na 23 mwaka huu. Timu
itakayofanikiwa kusonga mbele itacheza raundi ya pili dhidi ya Misri. Mechi ya
kwanza itachezwa nyumbani kati ya Oktoba 12, 13 na 14 mwaka huu wakati ya
marudiano itakuwa kati ya Oktoba 26, 27 na 28 mwaka huu.
Misri ni kati ya timu
17 zilizoingia moja kwa moja raundi ya pili. Nyingine ni Afrika Kusini, Algeria,
Burkina Faso, Cameroon, Congo Brazzaville, Cote d’Ivoire, Gabon, Gambia, Ghana,
Guinea, Mali, Rwanda, Senegal, Sierra Leone, Tunisia na Zambia.
0 comments:
Post a Comment